Home BUSINESS TANECU YAANZA SAFARI YA USHIRIKA IMARA KWA KUZINDUA VIWANDA VYA KUBANGUA KOROSHO

TANECU YAANZA SAFARI YA USHIRIKA IMARA KWA KUZINDUA VIWANDA VYA KUBANGUA KOROSHO

Chama Kikuu cha Ushirikia cha TANECU Ltd. kimeanza safari ya kuwa na ushirikia imara kwa kujenga kiwanda cha kubangua korosho Newala, mkoani Mtwara kilichogharimu shilingi bilioni 3.4.

Kiwanda hicho kimezinduliwa rasmi na Mhe. Hussein Bashe (Mb), Waziri wa Kilimo tarehe 1 Oktoba 2024 ambapo maelfu ya wakulima wameshuhudia kwa hamasa za uhakika wa soko la mavuno ya korosho zao.

Waziri Bashe ambaye yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi amekipongeza Chama Kikuu cha Ushirika cha TANECU Ltd. kwa kuwa mfano mzuri wa kuonesha ushirika unaozidi kuwa imara kwa kuhakikisha uwekezaji huo wa kiwanda ni wa wakulima wenyewe. “Naelekeza pia kijengwe kiwanda kingine kama hiki kule Tandahimba ili kiwe tayari wakati wa msimu wa mwaka ujao,” amesema Waziri Bashe.

Kiwanda cha TANECU kimegharimu shilingi bilioni 3.4 na kina uwezo wa kubangua tani 3,500 kwa mwaka. Mkakati ni kuwa na viwanda 20 vya Kubangua Korosho chini ya TANECU katika Mkoa wa Mtwara ambapo 10 vitajengwa Newala (tayari 1 kimezinduliwa); na 10 vitajengwa Tandahimba.

Previous articleDKT NCHIMBI AMESHIRIKI MAZISHI YA MAMA WA ABOUBAKARY LIONGO
Next articleMHE.BITEKO AWATAKA WANANCHI KULINDA MAENDELEO YA SHULE 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here