NA: HERI SHAABAN, (ILALA ).
SERIKALI imesema inatarajia kujenga barabara za kisasa Jimbo la Segerea katika mradi wa kuboresha Miundombinu ya Jiji UNDP .
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde wakati wa ziara iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la SEGEREA Wilaya Ilala kuangalia kero za Barabara .
“SERIKALI inatarajia kujenga barabara za kisasa katika mpango wake wa kuboresha Miundombinu ya Jiji UNDP awamu ya tatu katika Jimbo la segerea baadhi ya Kata zimeingizwa katika mradi huo.
Naibu Silinde alitaja Kata hizo ,Bonyokwa, Kisukuru ,Kimanga ,Kinyerezi Kimanga,alisema mradi huo wa UNDP ukikamilika wananchi wa eneo hilo watajivunia kwa kuwa na barabara za kisasa na Miundombinu yake
Kero hiyo imekuwa ikawasilishwa bungeni mara kwa mara na Mbunge wa Jimbo hilo, Bonnah Kamoli, huku akaianisha kuwa, baadhi ya kata ndani ya Jimbo la Segerea hazina hata barabara moja ya lami.
Akiongea wakati wa ziara yake ndani ya jimbo la Segerea, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, David Silinde amesema kuwa, serikali imesikia kilio cha wananchi na tayari imeshatoa fedha kwa ajili za ujenzi wa barabara mbalimbali jimboni humo.
Akiwa kata ya Bonyokwa, Naibu Waziri Silinde amesema, serikali imeshatoa kiasi cha shilingi milioni 150 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Zahanati ambayo ni miongoni mwa barabara korofi ndani ya kata hiyo.
Mbali na kiasi hicho cha fedha, Jiji la Dar es Salaam limeongeza kiasi cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa barabara, itakayojengwa kwa kiwango cha lami, barabara inayotajwa kumaliza changamoto ya wananchi wanayoitumia kwenda kupata huduma za afya.
Akiongea katika mkutano wake wa hadhara na wananchi wa Mtaa wa Karakata Kata ya Kipawa, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, David Silinde amewataka wananchi wa mtaa huo na Jimbo la Segerea kwa ujumla kutokuwa na wasiwasi katika suala la uboreshaji wa miundombinu, kwani serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni serikali ya vitendo na yenye kuangalia zaidi matokeo kuliko kuwekeza katika maneno.
Ameongeza kuwa, barabara zaidi zimeingizwa katika mpango wa DMDP na nyingine zimeongezwa hivi karibuni kutokana na umuhimu wake na hivyo zitajengwa kwa kiwango cha lami.
Akizitaja barabara zilizoongezwa katika mpango wa DMDP kuwa ni pamoja na barabara ya kutoka Baracuda hadi Maji Chumvi yenye urefu wa kilometa 3.5,barabara ya Majumba sita hadi Segerea, barabara ya Kijiwe Samli hadi Relini yenye urefu wa kilometa 1.2, barabara ya Umoja yenye urefu wa kilometa 3.
“Nawahakikishia serikali ya kupitia sisi wasaidizi wake, tunakwenda kuzifanya barabara zote za mijini na vijijini kupitika wakati wote.
Naye Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kamoli, ameishukuru Serikali pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaletea fedha katika jimbo hilo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati na maendeleo.
Akitolea mfano wa eneo korofi la Kipunguni Matembele ambapo sasa daraja linakwenda kujengwa na kuifanya barabara kupitika wakati baada ya kiongozi huyo Mkuu wa nchi kuwapa shilingi milioni 270 kwa eneo hilo pekee.
“Tumepewa shilingi milioni 270 kwa ajili ya kutengeneza daraja la Kipunguni Matembele, tunaishukuru serikali na Rais wetu Mama Samia Suluhu kwa kutongezea tena milioni 500 ambazo zitakwenda kutatua changamoto katika sehemu kubwa ya jimbo hilo” alisema Bonah.
Bonah alisema mara kwa mara bungeni nimekuwa nikipiga kelele kuhusu kero ya miundombinu ikiwemo miundombinu ya barabara katika jimbo letu la Segerea, kuna Baadhi ya kata hazina hata barabara moja ya lami, hivyo kwa kufikisha kilio changu serikalini, serikali imetusikia na matokeo yake ndio hayo ya ujenzi wa barabara hizo kuanza.
Naye Mhandisi wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Dar es Salaam, amesema kuwa, wao kama TARURA wamejipanga kikamilifu katika kutekeleza maagizo to serikali kwa kuziboresha na kukarabati barabara za zilizo chini yao na kuhakikisha zinapitika wakati wao ikiwemo barabara za jimbo la Segerea, huku akibainisha kuwa wataanza kufanya tathimini katika baadhi ya barabara kwa kukaa na wananchi na kufanya nao mikutano ili wakifikia makubaliano na kuridhia wako radhi kutengeneza barabara za mitaani huku changamoto kubwa kwao ikiwa ni fedha za kulipa fidia miongoni mwa watakaopisha ujenzi wa barabara hizo za mitaani.
MWISHO