Home LOCAL WADAU, SERIKALI WADHAMIRIA MATOKEO CHANYA UTEKELEZAJI WA VIPAUMBELE

WADAU, SERIKALI WADHAMIRIA MATOKEO CHANYA UTEKELEZAJI WA VIPAUMBELE

Na WMJJWM, Dar Es Salaam

Serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wanaoshughulikia huduma za Ustawi wa Jamii wamedhamiria kuhakikisha vipaumbele vilivyowekwa kutekeleza afua za Ustawi wa Jamii zinatoa matokeo.

Maamuzi hayo yamefikiwa wakati wa kikao cha pamoja kati ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum pamoja na wadau hao kilichofanyika jijini Dar Es Salaam Septemba 26, 2024.

Akifungua majadiliano hayo Katibu Mkuu, Wizara hiyo Dkt. Seif Shekalaghe, amewaomba wadau kujikita na kuwa na ushirikiano imara kwenye maeneo ya vipaumbele vya Serikali na namna ya kuyatekeleza.

Ili kuwa na ushirikiano imara, kuwe na mkutano wa wadau wa ustawi wa Jamii mara mbili kwa mwaka utakaojadili maeneo ya vipaumbele, utekelezaji wake na kuepuka kuingiliana kwa majukumu” amesisitiza Dkt. Shekalaghe.

Shekalaghe amevitaja vipaumbele vya Wizara kwa mwaka 2024/25 kuwa ni pamoja na kuimarisha Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto ngazi ya mitaa na vijiji, kutokomeza ukatili wa aina zote, Malezi na makuzi kupitia Programu ya MMMAM.

Vipaumbele vingine ni kuimarisha mfumo wa taarifa za Ustawi wa Jamii na kujenga uwezo wa uchambuzi na usimamizi wa data.

Baadhi ya wadau waliochangia mjadala huo akiwemo Mkrugenzi Mkaazi wa Shirika la PACT Levina Kikoyo wamesema kikao hicho kimekuja kwa wakati muafaka kwani itawasaidia kuingiza vipaumbele hivyo katika mipango bajeti zao ili ziendane na Serikali.

Previous articleTANROADS YADHAMIRIA KUBORESHA MIUNDOMBINU NCHINI
Next articleMFUMO WA KIDIGITALI WA AIRPAY NA ZEEA KUWARAHISISHIA WAJASIRIAMALI KUPATA MIKOPO KWA URAHISI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here