Home Uncategorized SKIMU 8 ZA UMWAGILIAJI KUNUFAISHA WANANCHI WA WILAYA YA NYASA

SKIMU 8 ZA UMWAGILIAJI KUNUFAISHA WANANCHI WA WILAYA YA NYASA

Wananchi wa Kijiji cha Lundo, Kata ya Lipingo, Wilaya ya Nyasa wamehakikishiwa kuwa na kilimo cha umwagiliaji cha uhakika kufuatia Serikali kuanza ujenzi na ukarabati wa skimu 8 za umwagiliaji eneo hilo. Wakulima hao wanalima zaidi mazao ya mpunga, muhogo, michikichi, mipera, kahawa na mengine.

“Changamoto zetu zaidi ni skimu za umwagiliaji zinahitajika kutokana na nyingine kupasuka, kuzibwa milango ya kupitisha maji na barabara kutokuwa nzuri kusafirisha mazao,” amesema Mhe. Eng. Stella Manyanya, Mbunge wa Nyasa.

Mbunge Manyanya ameongea mbele ya mkutano wa hadhara wa Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) wakati wa ziara yake ya kikazi tarehe 20 Septemba 2024, Wilaya ya Nyasa, Mkoani Ruvuma.

“Nimejionea umbali na umaskini wa ndugu zetu, nimeiona skimu ya Lundo yenye hekta 2,563 inayohijika kujengwa kwa kuwekea banio la maji, mifereji ya maji, barabara za mashamba na vidaraja vinavyogawa mashamba,” amesema Waziri Bashe. “Tutaweka utaratibu wa wakulima wote muweze kupata nafasi ya kulima kwenye skimu,” amesema Waziri Bashe. Gharama za ujenzi wa skimu ni shilingi bilioni 25.4.

Aidha, ameielekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) chini ya Mkurugenzi Mkuu Raymond Mndolwa mkandarasi akipatikana skimu ya Lundo, mkataba uongezwe ujenzi wa barabara ya skimu yenye ukubwa wa kilomita 2.5 na barabara ya Mawese ili zinufaishe wakulima kwa matumizi ya kusafirisha mazao. NIRC pia imeelekezwa kujenga ghala la kuhifadhi mpunga na mashine ya kukoboa mpunga.

Waziri Bashe amesema ujenzi wa skimu zote 8 utamilika kati ya miaka miwili na mitatu, ambapo pia ameielekeza Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kuweka ghala la mbolea za ruzuku.

Previous articleC-UNIT WANASEMA “ODIESHI” NI MUDA WA KUJIAMINI
Next articleKITUO CHA TARI NDENGU KUFUFULIWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here