Home LOCAL MHE.DKT.JAFO AWEKA JIWE LA MSINGI WA MRADI WA MAJI NACHINGWEA

MHE.DKT.JAFO AWEKA JIWE LA MSINGI WA MRADI WA MAJI NACHINGWEA

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi Mradi wa Maji Naipanga Wilaya ya Nachingwea ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Maalum Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Na.Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Selemani Jafo ametoa rai kwa wananchi wa Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi, kushirikiana, kusimamia utekelezaji miradi ya maendeleo kwa ufanisi ili ikamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Waziri Jafo, ameyasema hayo wakati akiweka Jiwe la Msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi wakati wa Ziara yake maalum katika wilaya ya Nachingwea Mkoa wa Lindi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ikiongozwa na Kauli Mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Dkt.Jafo amewataka wananchi kulinda, kutunza na kutumia vyema majengo na vifaa mbalimbali vilivyoweka kupitia Miradi hiyo na kuongeza kasi ya kutafuta hati ya ardhi kwa baadhi ya miradi ili kuhakikisha wanaendelea kupata huduma bora za afya, elimu, maji.

Nimeridhishwa na utekelezaji wa Miradi hiyo ya Maendeleo na kubainisha kuwa fedha zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa ajili ujenzi wa shule na vituo vya afya imetumika vyema kwa kuwa miradi hiyo imejengwa katika kiwango kinachohitajika.”amesema Dkt.Jafo

Aidha katika Ziara hiyo, Waziri Jafo akiwa ameambatana na Viongozi wa Chama na Serikali amekagua na kuweka Jiwe la Msingi katika Kituo cha Afya Lionja, Kituo cha Afya cha Kassim Majaliwa, Jengo la Kufulia, ICU, OPD, Maabara na Kichomea taka katika Hospitali ya Wilaya, ujenzi wa Bweni la Wanafunzi wenye uhitaji maalum Shule ya Msingi Chiwindi, Shule ya Msingi Nangunde pamoja na Mradi wa Maji wa Naipanga.

Katika hatua nyingine,akiongea na wananchi wa Naipanga pamoja na Wafanyabiashara wa Soko la Matunda Wilayani humo, Waziri Jafo aliwahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Sita itaendele kutatua changamoto mbalimbali walizonazo ili kuhakikisha kuwa huduma muhimu zinaendelea kutolewa kwa umma.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe. Mohammed Moyo ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo na kuahidi kuwa Wilaya yake itasimamia itekelezaji wa maagizo yote yaliyotolewa ilinkuhakikisha Miradi yote ya Maendeleo Wilayani humo inakamilika kwa wakati na kuanza kitoa huduma kwa wananchi katika muda uliopangwa.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo, akiweka Jiwe la Msingi katika Kituo cha Afya Lionja kilichopo Wilaya ya Nachingwea pamoja na kukagua ujenzi unaoendelea ikiwa ni mwendelezo wa Ziara Maalum Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiweka Jiwe la Msingi katika Shule ya Msingi Nangunde, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake maalum Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika Shule ya Msingi Nangunde,pamoja na kukagua ujenzi unaoendelea ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake maalum Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Selemani Jafo ,akiweka Jiwe la Msingi ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kassim Majaliwa na kukagua ujenzi unaoendelea pamoja na kuongea na Wananchi wa eneo hilo lililopo Wilaya ya Nachingwea ikiwa ni mwendelezo wa Ziara Maalum Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo, akizindia Jengo la ICU, Jengo la OPD, Jengo la Kufulia, Maabara na Kichomea taka na kutembelea Jengo la Chuo cha Uuguzi katika Hospitali ya Wilaya Wilaya ya Nachingwea ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Maalum Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiweka Jiwe la Msingi katika ujenzi wa Bweni la Wanafunzi wenye uhitaji maalum Shule ya Msingi Chiwindi Wilaya ya Nachingwea ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake maalum Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika ujenzi wa Bweni la Wanafunzi wenye uhitaji maalum Shule ya Msingi Chiwindi Wilaya ya Nachingwea ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake maalum Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiweka Jiwe la Msingi Mradi wa Maji Naipanga Wilaya ya Nachingwea ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Maalum Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi Mradi wa Maji Naipanga Wilaya ya Nachingwea ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Maalum Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko la Matunda Wilaya ya Nachingwea ikiwa ni mwendelezo wa Ziara Maalum Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na kusikiliza kero za wananchi wa Naipanga Wilaya ya Nachingwea ikiwa ni mwendelezo wa miara Maalum Mkoani Lindi inayolenga kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Awamu ya Sita chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone”

 

Previous articleCCM YASISITIZA UHUSIANO WA KIMATAIFA KUIMARISHA UCHUMI NA MAENDELEO YA WATU
Next articleNISHATI SAFI INAMUONDOLEA ADHA MTOTO WA KIKE – KIJAJI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here