DAR ES SALAAM.
Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Hassan Abas Rungwa amezitaka Halmashauri za Mkoa huo kuhakikisha zinaendesha shughuli zao kwa kuzingatia kanuni na taratibu ili kujiepusha na masuala ya kupata Hati Chafu au Hati zenye Mashaka kutoka kwenye Ripoti ya CAG.
Bwana Rungwa amesema hayo wakati wa kikao Cha Baraza la Madiwani la Jiji la Dar es salaam lililovunjwa na kikao Cha Baraza la Madiwani Kinondoni kilichoketi kujadili hoja na mapendekezo ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali CAG.
Akiwa kwenye kikao Cha Baraza la Madiwani la Jiji lililovunjwa ambalo kwa mujibu wa Ripoti ya CAG lilipata hati ya Mashaka, Bwana Rungwa amesema ni vyema kila Halmashauri ikajiadhari na hilo.
Ainda Rungwa amezitaka Halmashauri za Mkoa huo kuwatumia vizuri Wakaguzi wa ndani na kutoa ushirikiano kwa Wakaguzi pindi wanapohitajika kuonyesha vielelezo na nyaraka zinavyohitajika ili kuepuka Mambo ya hati Chafu.
Kikao Cha Baraza la Madiwani la Jiji lililovunjwa kimeketi kwenye Ukumbi wa Anatoglo na kikao Cha Baraza la Madiwani Kinondoni kimeketi ukumbi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ambapo vikao vyote viwili vimehudhuriwa na Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es salaam akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Amos Makalla.