|
Sehemu ya Washiriki wa warsha ya mafunzo ya haki za binadamu na utawala bora kwa watumishi wa sekta ya afya hospitali ya rufaa Dodoma wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayuko pichani) leo (Juni 25, 2021). |
Kamishna wa THBUB. Mhe. Dkt. Fatma Khalfan akitoa neno katika warsha ya mafunzo ya haki za binadamu na utawala bora kwa watumishi wa sekta ya afya wa hospitali ya rufaa Dodoma muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi. Warsha hiyo imefanyika ukumbi wa Bima ya Afya hospitalini hapo leo (Juni 25, 2021).
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Jabir Mussa Shekimweri ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya haki za binadamu na utawala bora kwa watumishi wa sekta ya afya hospitali ya rufaa Dodoma leo (Juni 25, 2021). Warsha hiyo ya siku moja imefanyika ukumbi wa Bima ya Afya ulipo hospitalini hapo.
|
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bwana Nabor Assey akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha ya mafunzo ya haki za binadamu na utawala bora kwa watumishi wa sekta ya afya hospitali ya rufaa Dodoma. Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo (Juni 25, 2021) katika ukumbi wa Bima ya Afya uliopo hospitalini hapo, na yamewahusisha takriban watumishi 30 wa kada mbalimbali.
Afisa Uchunguzi Mkuu wa THBUB, Bwana Yohana Mcharo akiwasilisha mada katika warsha ya mafunzo ya haki za binadamu na utawala bora kwa watumishi wa sekta ya afya wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma leo (Juni 25, 2021). Wengine katika picha ni watoa mada wenza kutoka THBUB, Bwana Peter Ntalika (wa kwanza kushoto) na Mwanyemi Bilali.
|
|
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dkt. Ernest Ibenzi (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Jabir Mussa Shekimweri leo (Juni 25, 2021) huku Kamishna wa Tume, Mhe. Dkt. Fatma Khalfan akishuhudia. Dkt. Ibenzi alipokea zawadi hiyo kwa niaba ya Muuguzi Mfawidhi wa hospitali hiyo, Bwana Stanley Zawadi hiyo ilitolewa kwa kiongozi huyo kutambua mchango wake mkubwa katika kukuza mahusiano na mashirikiano baina ya THBUB na hospitali hiyo ya rufaa. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Jabir Mussa Shekimweri (katikati) na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Fatma Halfani (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya haki za binadamu na utawala bora kwa watumishi wa sekta ya afya wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma. |