Home LOCAL MKUU WA MKOA IRINGA AWATAKA MADEREVA WA DALADALA KUWEKA...

MKUU WA MKOA IRINGA AWATAKA MADEREVA WA DALADALA KUWEKA VIFAA VYA TAKA

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga (mwenye koti jekundu) akifanya usafi Katika maeneo ya Manispaa hiyo Juni 28 mwaka huu. 


Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akizindua kampeni ya Usafi katika Manispaa hiyo Jana.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa ambaye ni Mkuu wa Idara Kitengo cha Mazingira ARDOM MAPUNDA akizungumza na Wananchi wa Manispaa ya Iringa katika uzinduzi wa usafi Juni 26/2021.

Wananchi na wataalam wakiwa katika picha na vifaa vya kubebea taka na Mkuu wa mkoa Iringa Queen Sendiga katika uzinduzi wa usafi Manispaa ya Iringa

NA: HERI SHAABAN, IRINGA.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Qeen Senndiga amezindua kampeni ya Iringa safi iliyofanyika Manispaa ya Iringa 

 baada ya matembezi ya hiyari ya kuokota taka taka kwa lengo la kuhamasisha jamii kushiriki katika masuala ya usafi na utuzaji wa Mazingira.

Mkuu wa mkoa Sendiga amewataka wananchi kutimiza wajibu wao wa  kufanya usafi  bila kusubiri kuhamasishwa na viongozi kwani usafi ni jukumu la kila mmoja.

Aidha ametoa wito kwa madereva wa daladala  na makondakta kuwa na vifaa vya kuhifadhia taka katika gari zao ili kuepusha mlundikano wa taka katika eneo la stendi kuu ya zamani unasababishwa na baadhi yao kutupa taka eneo hilo jambo ambalo linahatarisha  afya za wananchi.

“Leo tumezindua kampeni hii endelevu ya Usafi naomba daladala zote zitekeleze agizo hili wawe na vifaa maalum katika gari zao kwa ajili ya kuifadhia taka Manispaa yetu iwe safi na mkoa kwa ujumla “ alisema Sendiga

Alisema wananchi wanatakiwa kujenga tabia ya usafi katika maeneo yao  kila wakati wawe mabalozi wa usafi kwa kutoa elimu kwa jamii.

Kwa upande wake Kaimu MKURUGENZI wa MANISPAA YA IRINGA ARDOM  MAPUNDA  ambaye ni  Mkuu wa kitengo cha Mazingira  amesema anapokea maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa  ikiwemo kukamatwa kwa yeyote atakayeonekana kutupa taka hovyo na kuahidi kuyafanyia kazi mara moja.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Mapunda alisema watawachukulia hatua za kisheria wote wachafuzi wa mazingira ndani ya Manispaa kwa kuweka oparesheni Maalum ya usafi.

Mapunda alisema Iringa usafi inawezekana  amewataka Watendaji wa Kata na Wenyeviti  kushirikiana na Wananchi katika usafi ili Manispaa hiyo iwe safi.

Kampeni hiyo ya Iringa safi imezinduliwa na kuhudhuriwa na viongozi  mbali mbali wakiwepo Waheshimiwa Madiwani,wakuu wa idara na vitengo na wadau Nipe fagio pamoja na Envibright.

Mwisho.

Previous articleMAGAZETI YA LEO J.PILI JUNI 27-2021
Next articleYara Tanzania kushirikiana na serikali kuhamasisha matumizi bora ya mbolea na ukulima wa kisasa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here