Uongozi wa Yanga umeunda upya Baraza jipya la Wadhamini likiwa na sura mpya tatu kati ya watano.
Akitangaza uamuzi huo Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla amesema wameunda Baraza jipya la wadhamini litakaloanza kazi mara moja kama ambavyo katiba yao inaelekeza.
Akiwataja wajumbe hao Msolla amewataja wajumbe hao kuwa Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba ,Waziri Geoffrey Mwambe na Mbunge wa Kinondoni Abbas Tarimba.
Wengine ni Mama Fatma Karume mke wa Rais wa kwanza wa Zanzibar na Waziri wa ndani ya Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Kepteni George Mkuchika
“Hatutaweza kusema nani atakuwa Mwenyekiti wa Baraza hili wao wenyewe tunawaachia wamchague Mwenyekiti wao,” amesema Msolla.
Katika sura hizo Mwigulu Nchemba, Mwambe na Tarimba ndio wajumbe wapya wa Baraza hilo huku wenyeji wakiwa Mkuchika na Mama Karume