Kamishna Generali wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata akiongea na wadau wa kodi mkoa wa Arusha katika mkutano wao uliofanyika mkoani humo. |
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akifungua mkutano wa TRA na wadau wa kodi uliofanyika mkoani humo. |
Kelvin Remen meneja mazingira ya biashara kutoka TAHA alizungumzia mkutano huo wa wadau wa kodi na jinsi TRA inavyosaidia kutatua changamoto zinazotukabili katika suala zima la ulipaji wa kodi. |
Naibu Kamishna mkuu wa kodi wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Msafiri Mbibo akiongea na wadau wa kodi katika mkutano uliofanyika mkoani Arusha. |
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Kamishna Mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata amesema kuwa TRA ya sasa imebadilika kwani wanafanya kazi kwa uwajibikaji na uadilifu mkubwa ili waweze kuwahudumia walipa kodi vizuri kwa naendeleo ya nchi.
Kamishna Kidata aliyasema hayo katika kikao cha mamlaka hiyo na wadau wa kodi mkoa wa Arusha ambapo alisema kuwa wanafahamu serikali ya awamu ya sita inasisitiza maendeleo ya nchi yataletwa na wananchi wenyewe kupitia kodi hivyo watatekeleza jukumu walilopewa na serikali ili kuweza la kuweza kusimamia kwa kushirikiana na walipa kodi pamoja na kuwakumbisha wajibu wao.
“Lengo la mkutano huu ni kuwajulisha wadau wa kodi kuwa milango ya TRA ipo wazi na tupo tayari kuwahudumia vizuri kuliko jana kwa kuwasikiliza na kuchukua mawazo yenu na kuona uchumi wenu na uchumi wa nchi unakua,” Alisema Kamishna Kidata.
Aidha aliwasisitiza wadau wa kodia kuzingatia utunzaji wa kumbukumbu za biashara zao, kuimarisha matumizi sahihi ya mashine za kieletroni za kutoa risiti(EFD), pamoja na ulipaji kodi wa hiari kwani ni jambo linaloleta heshima kwa mlipa kodi yoyote.
“Tumeanza kampeni ya EFD kwa mkoa wa Arusha na mikoa mingine nasisitiza wananchi na wafanyabiashara kuwa na utamaduni wa kudai na kutoa risiti manunuzi yanapofanyia na hili ni suala la kisheria lakini pia tengenezeni mipango ya kulipa madeni ya nyuma na uandaaji wa ritani za kodi kwa usahihi,” Alisisitiza.
Pia alisisitiza matumizi ya stempu za ushuru katika bidhaa za Maji, Soda, pombe na Sigara kwa lengo la kuona uchumi unakua lakini pia kulinda utoaji wa bidhaa feki zinazoharibu sifa za bidhaa zao pamoja na kuwajibila kulipa Kodi kwa hiari kwani Tanzania ni kati ya nchi ambazo Kodi inayokusanywa inaenda kufanya shughuli za maendeleo.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akifungua mkutano huo alisema kuwa wataendelea kushirikiana na TRA kuhamasisha ulipaji kodi wa hiari ili kuweza kusaidia ufikiaji wa malengo yaliyokusudiwa kwa manufaa ya maendeleo ya nchi.
“Naamini kikao cha leo kitatidaidia kufika huko lakini Kama kiongozi nishauri upatikanaji wa EFD uwepo kwa urahisi na sio hadi mtu ajipange ndio apate hii itasaidia kuimarisha matumizi yake na kutatua changamoto ya ukwepaji wa kutumia mashine hizi kwa kisingizio Cha ugumu wa kupata,”iAlisema RC Mongela.
Pia aliagiza jamii ya walipa kodi kushirikiana na serikali na mamlaka ya mapato na kuondo dhana ya kuwa ulipaji kodi ni mfumo wa kunyanyasana bali wakubali kuwa sehemu ya maendeleo ya nchi.
Sambamba na hayo alisema kuwa bado mkoa wa Arusha unatumika Kama uchochoro wa wa bidhaa za kugushi(bandia) jambo linalohatarisha na kuteteresha uchumi wa mkoa ambapo yoyote atakayegundulika kuhusika na vitendo hivyo atachikuliwa hatua za kisheria.
Naye mmoja wa wadau wa kodi Kelvin Remen meneja mazingira ya biashara kutoka asasi kilele ya kilimo cha horticulture(TAHA) alisema kuwa mkotano huo utafanya kodi kulipwa kwa urahisi kwani ni fursa kubwa kwa wadau kueleza changamoto zao na kupatiwa ufumbuzi lakini pia wamekuwa wakifanya kazi kwa ukaribu na sekta binafsi wakituelewesha sheria na kanuni za ulipaji wa kodi.
sambamba na hayo pia alizungumzia hali ya biashara kwa Sasa ambapo alisema kuwa mazingira ya hali ya biashara wanaona yakizidi kuimarika kwani kumekuwa na changamoto ya Covid 19 ambayo imeadhiri sekta mbalimbali hasa ukizingatia mazao ya hoticulture ambayo wa nafanya uzalishaji hapa nchini lakini wanauza katika masoko ya kimatafa hivyo mazuio ya usafirisha na changamoto yaliyoikumba dunia yamewakumba na wao lakini kuna mapendekezo ambayo walishawasilisha kwa TRA na baadhi yameshafanyiwa kazi.