Home ENTERTAINMENTS WASANII WAKIKE KUMWAGIWA FURSA MAONESHO YA 24 ZIFF

WASANII WAKIKE KUMWAGIWA FURSA MAONESHO YA 24 ZIFF

 

NA: MWANDISHI WETU

FILAMU takribani 75 zinatarajiwa kuonyeshwa katika tamasha la Ziff linatakalofanyika Julai 21 mpaka 25 kisiwani Zanzibari.

Huu ni msimu wa 24 toka kuanzishwa kwa tamasha hili ambalo lina kutanisha wadau mbalbali wa sanaa ya filamu na muziki ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa tamasha hilo Martin Mhando, amesema tayari wamepokea kazi 75 kutoka kwa wasanii mbalimbali ambazo zitaonyeshwa, asilimia kubwa ya kazi hizo zimetengenezwa na wanawake.

“Mwaka huu tumepata kazi nyingi kutoka kwa wanawake hii inaonyesha ni jinsi gani wanajituma katika tasnia yetu filamu ya kwanza kuonyeshwa ina itwa Binti hii imetengenezwa na mwanadada Seko Shamte, ambaye ni mwalimu wa kuandaa filamu zenye maudhui ya kicho la kike hapa nchin ,” anasema Martn Mhando.

Mbali na filamu hizo kutakuwa na wasanii ambao watatumbwiza siku tatu za mwisho ambao ni Mbosso, Madj na Zenj Fleva.

Tamasha hilo litafanyima sehemu tofauti kisiwani humo ikiwemo Ngome Kongwe, Mambo Club na Maru maru 

Pia kutakuwa na utoaji wa tuzo kwa filamu ambazo zinashindanishwa zaidi ya 60 na kuendesha mafunzo kwa wasanii wa kike jinsi ya kutengeneza filamu zenye maudhui ya jicho la kike.

Previous articleHORN OF AFRICA YOUTH NETWORK PAID A COURTESY CALL TO EAC SECRETARY-GENERAL
Next articleTANZANIA KUIMARISHA UHUSIANO NA INDIA KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here