Home LOCAL VIJIJI 63 VYAFANYIWA MIPANGO YA MATUMIZI NA ARDHI CHAMWINO

VIJIJI 63 VYAFANYIWA MIPANGO YA MATUMIZI NA ARDHI CHAMWINO

Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip  Mpango akisalimiana na viongozi mara baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Mpwayungu wilaya ya Chamwino wakati wa kilele cha ziara yake ya siku nne mkoa wa Dodoma tarehe 22 Agosti 2024
Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amesema jumla ya vijiji 63 kati ya vijiji 73 vilivyokuwa katika mpango kwenye wilaya ya Chamwino mkoa wa Dodoma vimefanyiwa mipango ya matumizi bora ya ardhi.
Aidha, vijiji 10 vilivyosalia viko katika mchakato wa kufanyiwa mipango ya matumizi bora ya ardhi katika wilaya hiyo ya Chamwino.

Mhe. Pinda amesema hayo tarehe 22 Agosti 2024 katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mkwayungu wilayani Chamwino wakati kilele cha hitimisho ya ziara ya siku nne ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Mpango kukagua miradi ya maendeleo mkoani  wa Dodoma.

Mhe. Pinda, amesema kuwa  mpaka kufikia Disemba, 2024 vijiji vyote wilaya ya Chamwino vitakuwa vimeshafanyiwa mpango wa matumizi bora ya ardhi na kusisitiza kuwa, kimsingi migogoro ya mipaka ya vijiji imetatuliwa kwa kiwango kikubwa.

Mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji inaondoa changamoto kati ya mwananchi na mwananchi,wilaya na wilaya pamoja na changamoto nyingine za ardhi katika maeneo mengine”. Amesema Mhe. Pinda.

Aidha, ameongeza kuwa, kiasi cha Tshs. 1.5 bil kimetengwa na kutumika kwenye mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi ( LTIP) katika wilaya ya CHAMWINO.

Sambamba na hilo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema,

Vijiji 27 vimepimwa na kutayarishiwa vyeti ya vijiji huku vipande vya ardhi vilivyotambuliwa kwa ajili ya kutoa Haki za hatimiliki za Kimila ( CCROs) ni 20,455.

Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip  Mpango akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika scheme ya umwagiliaji katika kijiji cha Ndogowe wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma tarehe 22 Agosti 2024. Kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi Mhe, Geophrey Pinda.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip  Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika scheme ya umwagiliaji katika kijiji cha Ndogowe wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma tarehe 22 Agosti 2024. Kushoto aliyesimama ni Naibu Waziri wa Ardhi Mhe, Geophrey Pinda.
(PICHA NA WIZARA YA ARDHI)
Previous articleRAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI KWENYE MRADI WA SULUHU SPORTS ACADEMY KIZIMKAZI ZANZIBAR.
Next articleUWEKEZAJI UNAOFANYWA NA SERIKALI  KATIKA SEKTA YA UMWAGILIAJI UNAENDA KUMALIZA NJAA NCHINI -DKT MPANGO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here