Home LOCAL NAIBU WAZIRI UMMY, APOKEA JEDWALI LA UCHAMBUZI LA SHERIA NDOGO

NAIBU WAZIRI UMMY, APOKEA JEDWALI LA UCHAMBUZI LA SHERIA NDOGO

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo Mhe. Ramadhan Suleiman Ramadahan akiongoza kikao cha Kamati Ndogo ya Bunge ya Sheria Ndogo katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Ummy Nderiananga amepokea Jendwali la Uchambuzi la Sheria Ndogo za Mwaka 2024 katika Mkutano wa Kumi na Tano, Kikao cha sita cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zimewasilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo Mhe. Ramadhan Suleimani Ramadhan.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akipokea jendwali la uchambuzi la Sheria Ndogo kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya sheria Ndogo Mhe. Ramadhan Suleimani Ramadhan.

Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma Leo tarehe 16/ 08/ 2024 ambapo amesema mafanikio ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) yanatokana na ushirikiano ambao umekuwa ukitolewa na Kamati ya Bunge ya Sheria ndogo.

Naomba niwahakikishie kamati; nimepokea jedwali hili na tutawasilisha kwa Wizara zinazohusika ili zije zilete majibu, naomba tuendele kupata ushirikiano wakati wizara hizo zitakapokuja kuwasilisha,” alisema Naibu Waziri Ummy.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza wakati wa upokeaji wa Jendwali la Uchambuzi la Sheria Ndogo katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.

Previous articleWAZIRI MKUU KASIMU MAJALIWA AKIFANYA ZIARA MAALUM KUBORESHA MAHUSIANO KATI YA CUBA NA TANZANIA
Next articleWAKULIMA WA TUMBAKU WAPEWA MBINU KUONGEZA UZALISHAJI.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here