Home LOCAL WANASIASA TUCHUNGE NDIMI ZETU-NCHIMBI

WANASIASA TUCHUNGE NDIMI ZETU-NCHIMBI

 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amewataka wanasiasa nchini, kutumia vizuri ndimi zao na kamwe wasitoe matamshi ambayo yanaweza kuhatarisha amani na utulivu nchini.

 

Balozi Dk. Nchimbi ameyasema hayo Jumanne Agosti 13, 2024 alipokua akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Uwanja, Geita Mjini.

Balozi Nchimbi amesema wanasiasa wasijisahau katika kuchagua maneno yanayoweza kuhatarisha amani ya nchi yetu, na kuongeza kuwa wako watu ndani ya wanajisahau, hivyo amewaomba Watanzania wasijisahau.

Wana CCM na Wanasiasa wa vyama vingine wachague maneno wanayoyatumia, kwani wote wanajenga Nchi moja inayoitwa Tanzania ambayo wana wajibu wa kuipenda na kuitumikia kwa nguvu zote.”,amesema Nchimbi

Dkt. Nchimbi anaendelea na ziara yake ya siku tatu mkoani Geita,yenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi, kuangalia Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuimarisha uhai wa Chama cha Mapinduzi.

Katika ziara hiyo Balozi Dkt.Nchimbi ameambatana na Ndugu Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) – Oganaizesheni, Ndugu Amos Gabriel Makalla, Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo na Ndugu Rabia Abdalla Hamid, Katibu wa NEC – Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

Previous articleSTARTIMES KUENDELEA KUUNGA MKONO LIGI YA CHAMPIONSHIP
Next articleWAZIRI MKUU AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA CUBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here