Home LOCAL WAZIRI KOMBO AJITAMBULISHA KWA RAIS WA ZANZIBAR DKT. HUSSEIN MWINYI

WAZIRI KOMBO AJITAMBULISHA KWA RAIS WA ZANZIBAR DKT. HUSSEIN MWINYI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), pamoja na Manaibu wake, Mhe. Cosato Chumi (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Dennis Londo (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Masuala ya Afrika Mashariki; wamefanya ziara ya kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Ikulu Zanzibar.

Katika utambulisho huo, viongozi hao wamemuhakikishia Rais Mwinyi kuendelea kushirikiana kwa karibu na kuhakikisha kuwa maslahi ya pande zote mbili—Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar—yanapewa kipaumbele. Ziara hii ni hatua muhimu katika kuimarisha umoja na mshikamano kwa manufaa ya wananchi wote wa Tanzania, ambapo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni Wizara ya Muungano.

        

Previous articleZAIDI YA WANANCHI 300 WAELIMISHWA EWURA INAVYOSHUGHULIKIA MALALAMIKO
Next articlePITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 10, 2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here