DAR ES SALAAM
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi, amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kuende;eza mikakati yake ya kuwasaidia wananchi mwenye kipato cha chini kumiliki nyumba.
Waziri Ndejembi ameyasema hayo leo Agosti 9,2024 alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa malengo ya kuanzishwa kwa Shirika hilo lililoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere ni kujenga nyumba zenye viwango vya hali ya juu ambazo pia zinaweza kununuliwa na wananchi wenye kipato cha chini.
Amesema kuwa NHC inapaswa kuanzisha utaratibu wa kulipa kiasi fulani cha asilimia ya gharama ya Nyumba na kuruhusu mteja huyo kuanza kuishi huku akiwa analipa kiasi kidogo cha fedha kila mwezi mpaka atakapomaliza deni lake.
Aidha, Mhe. Ndejembi amelipongeza Shirika hilo kwa kuanza utekelezaji wa mradi wa Samia Housung Scheme wenye lengo la kujenga Nyumba 5,000, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza mradi huo katika maeneo ambayo bado hayafikiwa na yenye uhitaji.
Mhe. Ndejembi ametoa wito kwa menejimenti ya NHC kuhakikisha hakuna wizi wa vifaa vya ujenzi wakati wa utekelezaji wa miradi ya Shirika nakwamba kwa kufanya hivyokutasaidia thamani ya Nyumba kuendana na gharama halisi za ujenzi.