Home Uncategorized GAVANA TUTUBA: WAKOPESHAJI WANAPASWA KUTOA NAKALA YA MASHARTI YA MKOPO

GAVANA TUTUBA: WAKOPESHAJI WANAPASWA KUTOA NAKALA YA MASHARTI YA MKOPO

DODOMA.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Emmanuel Tutuba, amewataka wakopeshaji nchini kuhakikisha wanatoa nakala ya masharti yenye lugha rahisi ya mikopo wanayotoa kwa wananchi, ili mkopaji aweze kuelewa masharti ya mikopo kabla hajakopa.

Gavana Tutuba ameyasema hiyo alipotembelea Banda la BoT Jijini Dodoma, kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini humo.

Amesema kuwa Mkopaji anapaswa kujiridhisha na masharti ya mkopo, matumizi ya mkopo pamoja na uhimilivu wa kurejesha mkopo huo.

ā€œTunasisitiza mkopaji lazima asome masharti na ajiridhishe kujua kama anaweza kuyamudu. Kwani kuna baadhi ya wakopeshaji wasio waadilifu wanaweka masharti kwa kificho ili mkopaji asiyafahamuā€,amesema Gavana Tutuba.

Aidha, mewataka wakopaji wasichukue mkopo mkubwa kupita uwezo wao, lakini pia fedha wanazokopa kuzielekeza kwenye shughuli za kiuchumi ili waweze kurejesha mkopo huo.

ā€œElimu ya fedha ni suala mtambuka na nilaumuhimu sana. Hapa kwenye maonesho tunaendelea kutoa elimu ili kumuwezesha mtu kutafuta pesa kwenye njia halali aweze kuzitunza lakini awe na nidhamu ya pesaā€,Amesema.

Ameongeza kuwa BoT wametoa miongozo kwa taasisi ndogo za fedha ambayo inamtaka mtu anapoenda kukopa hata kama hana elimu ya fedha anapaswa azingatie viwango ambavyo ni himilivu kulingana na mazingira ya uchumi.

Sambamba na hayo amesema katika maonesho hayo wanatoa elimu ya namna mifumo ya fedha inavyofanyakazi, lakini pia kuonesha namna uchumi ulivyokuwa imara .

ā€œTumeshiriki katika maonesho haya kuwaonesha wananchi namna uchumi wetu ulivyokuwa imara na unavyoendelea kusimamia vizuri taratibu zote za mabenki na mifumo ya kifedhaā€.Amesema.

 

Previous articleMAFANIKIO MAKUBWA DAWASA, WAFIKISHA ASILIMIA 93 UTOAJI HUDUMA YA MAJIĀ 
Next articleDCEA YATOA ELIMU KWA WANANCHI NANENANE DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here