DAR ES SALAAM.
– Amshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti ya barabara za TARURA Nchi nzima.
– Bajeti ya Ujenzi wa Barabara TARURA Dar es salaam imepanda kutoka Bilioni 25 Hadi Bilioni 40 na TARURA Taifa kufikia bilioni 300.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo August 10 ameshuhudia awamu ya kwanza ya utilianaji sahihi wa mikataba 41 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 14.1 kwaajili ya Ujenzi wa Barabara za Mkoa wa Dar es salaam na kuwataka Wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha Miradi kwa wakati na kwa kiwango.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa hafla ya utilianaji sahihi mikataba baina ya TARURA na Wakandarasi ambapo amesema mafanikio haya yote ni matokeo ya kazi kubwa na nzuri ya Serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan Katika utatuzi kero za Wananchi.
Aidha RC Makalla amewaelekeza DAWASA, TANROAD, TARURA, TTCL na TANESCO kufanya kazi kwa pamoja ili kuondoa tatizo la miradi kutomalizika kwa wakati Kutokana na Taasisi husika kuchelewa kuhamisha miundombinu.
Pamoja na hayo RC Makalla amewaelekeza TANROAD na TARURA kuhakikisha wanasimamia utunzaji wa miundombinu ya Barabara ikiwa ni pamoja na Usafi, ukarabati na uwekaji wa Vibao vya kuzuia biashara Kwenye eneo la hifadhi ya Barabara.
Hata hivyo RC Makalla ameonyesha kufurahishwa na ongezeko la bajeti ya Ujenzi wa Barabara Dar es salaam kutoka Shilingi bilioni 25 adi bilioni 40 na Nchi nzima kufikia Bilion 300.