Home BUSINESS UDOM WAFURAHISHWA NA MUITIKIO MKUBWA WA WANANCHI

UDOM WAFURAHISHWA NA MUITIKIO MKUBWA WA WANANCHI

DODOMA

Chuo Kikuu Cha Dodoma wamefurahishwa na mwitikio mkubwa wa Wananchi wanaotembelea banda la Chuo hicho kwa ajili ya kuona bidhaa, kupata elimu ya masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kulima kilimo cha kisasa, kupima afya pamoja na ushauri wa chakula tiba ili waweze kuboresha maisha yao.

Akizungumza leo Agosti 6, 2024 katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika Nzuguni jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Kitengo Cha Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu Cha Dodoma Bi. Rose Joseph, amesema kuwa tangu maonesho hayo yaanze banda hilo limekuwa na idadi kubwa ya wananchi kwa ajili ya kupata elimu ambayo ni msaada katika kutatua changamoto zinazowakabili.

Bi. Joseph amesema kuwa watanzania kwa sasa wameelimika kutokana wamekuwa na hamasa ya kujifunza ikiwemo kuacha ulaji holela na kwenda katika ulaji wenye manufaa ambao utawasaidia kuboresha afya ili kupunguza maradhi yanayotokana na mfumo wa maisha ya kila siku.

“Wananchi wana mwamko wa kujua afya zao katika masuala ya maambukizi ya virus vya ukimwi ili waweze kujua namna ya kuishi kama watakuwa na maambukizi pamoja na kuchukua tahadhari” amesema Bi. Joseph.

Amesema kuwa elimu imeendelea kutolewa na wataalam katika banda la Chuo Kikuu Cha Dodoma, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi wa kulinda afya zao.

Previous articleRAIS SAMIA APEWA MAUA YAKE, KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YAWA MKOMBOZI WA WANYONGE
Next articleUDOM WAFANIKIWA KUBUNI MIFUMO YA TEHAMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here