Amesema hayo katika maonesho ya ya Kimataifa ya Kilimo(Nanenane) yanayofanyika jijini Dodoma katika viwanja vya Nzuguni mkoani humo, lengo ni kufanya kazi nzuri ya ujenzi wa barabara na madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe ili kupunguza gharama na kupata barabara imara katika kuwasaidia wananchi kuondokana na changamoto mbalimbali za usafiri.
“Jambo kubwa tunalolifanya sisi kama TAMURA ni kufanya ujenzi pamoja na ukarabati kwa kila kilometa katika barabara zetu nchini
Katika maonesho haya tumekuja na teknolojia ya kujenga madaraja na barabara kwa kutumia mawe kama unavyojua kwamba sisi ndiyo taasisi ambao inawawezesha wananchi hasa vijijini kufika sehemu ambazo hazifikiki.
Maana yangu ni kwamba kuwawezesha wakulima kusafirisha mazao yao kutoka vijijini kwenda mpaka mjini na kusafiri kwa urahisi mara wanapopata changamoto ya kuugua wakati wanapokwenda kutafuta matibabu katika zahanati na vituo vya afya.
Amesema kwa TARURA kutengeneza barabara na madaraka inawarahisishia wananchi Vijijini kutoa mazao yao kutoka mashambani mpaka sehemu ambapo kuna magari ili kusafirisha mazao hayo kupeleka sokoni.
Tumeweza kufanya ukarabati zaidi wa madaraja na barabara ili kuwasaidia wananchi katika kufanya shughuri zao za kiuchumi ikiwemo usafirishaji wa mazao na kuwasaidia katika huduma za kiafya mfano wakina mama wajawazito kupata huduma kwa urahisi na haraka.
Tangu TARURA ilipoanzishwa tumejenga madaraja 250 nchi nzima na mkoa wa Kigoma ndiyo unaoongoza.
Na ili kuounguza gharama za ujenzi na kufikia huduma kwa haraka madaraja yamejengwa kwa mawe mfano mikoa ya Mwanza,Kigoma,Morogoro ni baadhi ya mikoa iliyonufaika na teknolojia hiyo.
“Lengo ni kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa haraka kwa kutumia tekinolojia mbadala,kuna teknolojia nyingi ikiwemo Ekoloji mfano Dodoma imejenga madaraja kwa tekinorojia hii.”amesema Ngeleja
Catherine Sungura ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha ulUhusiano na Mawasiliano Wakala wa Barabara za vijijini na mijini TAMURA ameongeza kwa kusema kuwa TARURA madaraja mengi hasa vijijini na juzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amfungua daraja ambalo limetengenezwa na TARURA lengo likiwa kuwasaidia wananchi kufanya shughuli zao kwa urahisi ikiwemo kwenda kufuata huduma za kijamii”.amesema.