Shirika la uwakala wa meli Tanzania. (TASAC) kupitia. Mkoa wa kigoma imepokea taarifa ya kupotea kwa jahazi la mizigo liitwalo MV AMINA ambalo limesajiliwa na TASAC kwa namba za usajili TKG 002449.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na TASAC imeeleza kuwa Shirika hilo kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali za kiserikali zmeratibu utafutaji na uokozi pamoja na jeshi la polisi na wanamaji katika kufanikisha upatikanaji wa Jahazi hilo.
Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa jahazi hilo lenye urefu wa mita 18 lilikuwa na mabaharia nane kutoka nchini Tanzania, iliondoka kwenye bandari ya Ilagala Tanzania saa 10:00 jioni tarehe 27 2024 huku likitarajiwa kuwasili katika bandari ya kalemine nchini Kongo.
Kutokana na uchunguzi ambao umefanyika imebainika kuwa kumekuwa na changamoto ya mtambo uliopelekea Jahazi hilo kupoteza mwelekeo wa mabaharia waliokuwa kwenye Jahazi hilo mbao walipelekwa kwenye mwalo wa sunuka kigoma.
Katika hatua nyingine TASAC imewaomba wananchi na wadau katika kutoa taarifa kupitia kwenye kituo cha kuratibu na utafutaji na uokoaji (MRCC) pindi dharura zinapotokea majini.