Home BUSINESS WATUMISHI WIZARA YA FEDHA WAHIMIZWA KUENDELEA KUCHAPA KAZI

WATUMISHI WIZARA YA FEDHA WAHIMIZWA KUENDELEA KUCHAPA KAZI

PIX%2B1%2B%25286%2529
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akizungumza wakati akifungua Kikao cha Watumishi wa Wizara ya Fedha kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), jijini Dodoma, ambapo amewaagiza watumishi kuimarisha mfumo wa ukusanyaji wa mapato na kuratibu upatikanaji wa fedha ili kutoa fedha kwa wakati kwa miradi yote iliyoidhinishwa na Bunge.
PIX%2B2%2B%25285%2529
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akizungumza wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) kufungua Kikao cha Watumishi wa Wizara, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), jijini Dodoma, ambapo ameeleza kuwa lengo la kikao hicho ni kushirikishana masuala mbalimbali ya kiutendaji pamoja masuala mengine yanayogusa maisha ya watumishi nje ya utumishi wa Umma.
PIX%2B3%2B%25284%2529
Watumishi wa Wizara ya Fedha, wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (hayupo pichani), wakati akifungua Kikao cha Watumishi wa Wizara ya Fedha kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), jijini Dodoma.
PIX%2B4%2B%25286%2529
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa, akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Fedha, wakati wa Kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), jijini Dodoma, ambapo ameipongeza Wizara kwa kufanikisha kikao hicho kikijumuisha kwa mara ya kwanza viongozi wa Taasisi za Wizara na kutoa rai kuwa vikao hivyo vijumuishe watumishi wote wa Taasisi za Wizara ili kuwa na uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa majukumu.
PIX%2B5%2B%25283%2529
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali (IAG), Bw. Benjamin Magai, akizungumza jambo wakati wa Kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), jijini Dodoma, ambapo ameupongeza uongozi wa Wizara kwa kuitisha kikao hicho kwa kuwa kitachochea ufanisi wa kazi.
PIX%2B6%2B%25284%2529
Mwandishi Mwendesha Ofisi Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Mwamanga, akichangia jambo wakati wa majadiliano ya Kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), jijini Dodoma, ambapo kilijumuisha Menejiment ya Wizara, Wakuu wa Taasisi za Wizara a Fedha, Hazina Ndogo za Mikoa, pamoja na watumishi wa Wizara kwa ajili ya kushauriana na kubadilishana uzoefu juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Wizara, Taasisi na Serikali kwa ujumla.
PIX%2B7%2B%25283%2529
Meza Kuu ikiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (Katikati), na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (watatu kushoto), wakifuatilia majadiliano na maswali kutoka kwa watumishi wa Wizara ya Fedha, wakati wa Kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), jijini Dodoma, ambapo kilijumuisha Menejiment ya Wizara, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara, Wakuu wa Hazina Ndogo za Mikoa, pamoja na watumishi wa Wizara kwa ajili ya kushauriana na kubadilishana uzoefu juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Wizara, Taasisi na Serikali kwa ujumla. Wengine katika picha ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali (IAG), Bw. Benjamin Magai (wa kwanza kushoto), Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa (wa pili kushoto), Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni, Bw. Japhet Justine (wa tatu kulia), na Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Prof. Hozen Mayaya.
PIX%2B8%2B%25281%2529
Meza Kuu ikiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (Katikati), na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Menejimenti ya Wizara ya Fedha, baada ya kumalizika kwa Kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), jijini Dodoma, ambapo kilijumuisha Wakuu wa Hazina Ndogo, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na watumishi wa Wizara hiyo kwa ajili ya kushauriana na kubadilishana uzoefu juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Wizara, Taasisi na Serikali kwa ujumla.
PIX%2B9
Meza Kuu ikiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (Katikati), na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, baada ya kumalizika kwa Kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), jijini Dodoma, ambapo kilijumuisha Menejimenti ya Wizara, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara, Wakuu wa Hazina Ndogo, na watumishi wa Wizara kwa ajili ya kushauriana na kubadilishana uzoefu juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Wizara, Taasisi na Serikali kwa ujumla.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)


Na. Saidina Msangi na Farida Ramadhani, WF, Dodoma

Watumishi wa Wizara ya Fedha wameagizwa kuimarisha mfumo wa ukusanyaji wa mapato na kuratibu upatikanaji wa fedha ili kutoa fedha kwa wakati kwa ajili ya kutekeleza miradi yote iliyoidhinishwa na Bunge.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Fedha kwa niaba ya Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akifungua kikao cha watumishi na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), jijini Dodoma.
Alisema kuwa ni muhimu watumishi hao kutekeleza majukumu yao na maelekezo yanayotolewa na Serikali kwa wakati ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi kwa wakati yatokanayo na mjadala wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2024/25.
‘‘Ni muhimu kuwa mfano katika kuzingatia miongozo ya usimamizi wa mali na fedha za Umma, hususan katika kufungamanisha mahitaji yetu na bajeti iliyoidhinishwa na Bunge pamoja na kuimarisha mfumo wa ushirikishaji, uratibu na kufanya kazi kwa karibu na wadau wetu ili kuongeza ubora wa huduma zetu kwa wateja wa ndani na nje ”, alisisitiza Mhe. Chande.
Aliwaelekeza watumishi hao kutumia taaluma zao katika kushauri na kufanya maamuzi kwa wakati kwa maslahi mapana ya Taifa pamoja na kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyopo ili kuimarisha mfumo wa utawala bora na utawala wa sheria.
Aidha, aliwaagiza Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo, kuendelea kusimamia majukumu waliyopewa katika Taasisi wanazoongoza na kuongeza ubunifu na weledi ili kuweza kuchangia fedha katika mfuko Mkuu wa Serikali.
Alisema ni muhimu kusimamia majukumu yao kwa kuzingatia sheria na kanuni, mali na fedha za Serikali ikiwemo kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za Umma katika Ununuzi. 
‘‘Nendeni mkatekeleze kwa ufanisi Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023 na Kanuni zake pamoja na kutumia Mfumo wa NeST, tutimize viapo na wajibu wetu katika suala la usimamizi wa mali na fedha za Umma,’’aliagiza Mhe. Chande.
Mhe. Chande alitoa wito kwa watumishi hao kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kushiriki katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura ili kuweze kutumia haki zao wakati wa uchaguzi mkuu kuchagua viongozi wanaowataka na kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo katika Taifa letu ili shughuli za kiuchumi na kijamii ziendelee kuimarika.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu wa wizara hiyo Bi. Jenifa Christian Omolo alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kushirikishana masuala mbalimbali ya kiutendaji pamoja masuala mengine yanayogusa maisha ya watumishi nje ya utumishi wa Umma.
‘‘Lengo la kujumuisha masuala ya maisha ya watumishi nje ya utumishi wa Umma ni kukumbushana kuwa sisi watumishi ni sehemu ya Umma, na pia inawezekana leo ni watumishi wa Umma lakini kesho tukawa raia kama raia wengine nje ya utumishi wa Umma’’alieleza Bi Omolo.
Akizungumzia utekelezaji wa majukumu ya wizara Bi. Omolo alisema kuwa Wizara imeendelea kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa mpango na bajeti ya 2023/24, bila kusahau changamoto mbalimbali zilizosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Alisema wizara imeendelea kutoa huduma kwa wateja kwa mujibu wa muundo na mgawanyo wa majukumu ya Serikali, kubuni na kusimamia utekelezaji wa Sera za Uchumi jumla, Fedha na Ununuzi wa Umma pamoja na kusimamia ukusanyaji wa mapato na utaratibu wa upatikanaji wa fedha kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo.
‘‘Tumeendelea kuratibu upatikanaji wa fedha na kuimarisha uhusiano wa masuala ya fedha kwa Taasisi za kikanda na Kimataifa, kutekeleza maelekezo ya viongozi na kushiriki katika shughuli mbalimbali za pamoja za kitaifa ikiwemo michezo ya Mei Mosi, SHIMIWI, maonesho ya SABASABA, Nanenane n.k;’’, alifafanua Bi. Omolo.
Kikao hicho cha wafanyakazi kilijumuisha Wakuu wa Hazina Ndogo, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na watumishi wa wizara hiyo kwa ajili ya kushauriana na kubadilishana uzoefu juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Wizara, Taasisi na Serikali kwa ujumla.
Naye Mtakwimu Mkuu wa Serikali Bi. Albina Chuwa ameipongeza wizara kwa kufanikisha kikao hicho kikijumuisha viongozi wa Taasisi za wizara na kutoa rai kuwa vikao hivyo vijumuishe watumishi wa Taasisi za wizara ili kuwa na uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa majukumu.
Previous articleSSI ENERGY TANZANIA LTD YASAINI MKATABA WA UJENZI WA MRADI WA UMEME JUA WA MEGAWATI 100MW KAHAMA
Next articleRAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here