“Mimi ni Waziri ninayeshughulika na Sekta ya Nishati, tulikua na shida ya umeme kwenye nchi yetu, umeme unakatika kwa sababu umeme mdogo mahitaji ni mengi, Mama Samia amesimamia, sasa hatuna mgawo wa umeme na tunaendelea kuimarisha miundombinu ya umeme,” amesisitiza Dkt. Biteko.
Ameongeza kuwa maono ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuwaona Watanzania wanapata maendeleo katika nyanja za kiuchumi na kijamii nchini na ndiyo sababu ya kusukuma maendeleo kwa haraka katika kipindi chake cha uongozi ndani ya miaka mitatu ambapo amefanya kila kitu kwa viwango vya juu.
“Sisi wake anatuagiza wakati wote tukawasikilize wananchi kero zao, tusikilize shida zao na mimi nimekuja hapa kuwaambia Rais Samia anawapenda, anawathamini ataleta maendeleo zaidi,” ameongeza Dkt. Biteko.