Home LOCAL DC ILALA AMETOA AGIZO KWA WATUMISHI JIJI WANAOKWAMISHA MIRADI YA SERIKALI...

DC ILALA AMETOA AGIZO KWA WATUMISHI JIJI WANAOKWAMISHA MIRADI YA SERIKALI KUWAKAMATA

 NA: HERI SHAABAN (ILALA)

MKUU wa Wilaya ya Ilala Arch ,Gw’wilabuzu Ludigija ametoa agizo kwa Watumishi wa halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, ambao wanakwamisha miradi ya Serikali kuwakamata   kuwaweka ndani.

Mkuu wa Wilaya Ilala Ludigija aliyasema hayo Leo katika ziara ya kustukiza Vingunguti kukagua machinjio ya nyama Vingunguti na mradi wa mabucha ya nyama ya kisasa ambayo mkataba wa ujenzi wake umeisha lakini mpaka leo ujenzi wake unasuasua .

“Ninaagiza kwa Watumishi wa halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wanaokwamisha miradi ya Serikali nitawaweka ndani nawapa wiki moja miradi huu wa mabucha ya nyama uwe umemalizika wafanyabishara waanze kuyatumia mara moja” alisema Ludigija .


Mkuu wa Wilaya Ludigija alisema ujenzi wake mabucha hayo ya kisasa yaliotakiwa kukabidhiwa leo Agosti 24 mwisho wa mkataba lakini bado kwisha .

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya Ilala Ludigija ameagiza MZABUNI  wa miradi  wa mabucha ya kisasa Vingunguti kujisalimisha Kituo cha Polisi Buguruni kujieleza kama kosa lipo kwa upande wake  atachukuliwa hatua kama tatizo kwa Watumishi wa halmashauri ya jiji basi atawaweka ndani kwa kukwamisha miradi wa mabucha.

Mkuu wa Wilaya Ilala ameshangazwa mradi huo wa miezi miwili kuchukua miezi nane bila mafanikio  kutokana na kudaiwa kuwapa tenda watu wasio na uwezo.

Wakati huo huo Mkuu wa  Wilaya Ilala ametoa SAA 48 akimwagiza Mkuu wa Idara ya Mifugo wa Halmashauri ya Jiji ,Afisa Afya na Afisa Mtendaji wa Kata Vingunguti kuwaondoa wafanyabiashara wa kuuza nyama na Utumbo waliopo Barabara ya Vingunguti wamishiwe katika maeneo yaliotengwa ambayo yatauza nyama sehemu Salama kutokana na eneo hilo ambalo wanauza bidhaa zao si salama kwa walaji nyama pia wanaharibu miundombunu ya Barabara.

Kwa upande wake Mhandisi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Chacha Magori alisema Mzabuni aliyepewa tenda hiyo uwezo wake mdogo hivyo achukuliwe hatua .

MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam amemshauri Mkuu wa Wilaya Ilala Ludigija kuwamisha baadhi ya Watumishi wa halmashauri hiyo kwa kudaiwa kufanya kazi kwa mazoea na kukwamisha miradi ya Serikali.

Mwisho.

Previous articleMAGAZETI YA LEO J.TANO AGOSTI 25-2021
Next articleHABARI KUU KATIKA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 26-2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here