Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho, akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa (REA) wakati hafla ya kuwasha umeme katika kitongoji cha Shuleni kilichopo kijiji cha Chihurungi.
Na Mwandishi wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jensita Mhagama ametaka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha wanaweka mkakati mzuri wakusaidia kusambaza umeme vijijini kwa kwa Taasisi za Serikali na Dini.
Waziri ametoa kauli hiyo wakati hafla ya kuwasha umeme katika kitongoji cha Shuleni kijiji cha Chihurungi iliyofanyika katika Halmashauri ya wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma leo tarehe 14/07/2024.
Halmashauri yetu sasa imebakiza vijiji vinne, na vijiji vienyewe mpaka mwezi wa tisa mwaka huu, vijiji vyote vitakuwa vinawaka umeme ikiwemo kijiji cha Nambendo kilichopo pembezoni ambacho tayari utandazaji wa nyaya za umeme unaendelea.
Waziri amesema, “tunao moyo wa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, huku tukiendelea kuomba vitongoji vilivyoongezwa kuwekewa umeme vipate umeme haraka.”
Wananchi wa Chihurungi umeme huu mkautumie vizuri ili kuleta faida fungamanishi za kiuchumi, ikiwemo viwanda vya chuma, na viwanda vya kutengeneza magrili, alifafanua
Awali Wakala wa Nishati Vijijini na Msimamizi wa Mradi wa (REA) Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Robert Ndule amesema Chihurungi ni moja ya vijiji 28 vilivyokuwa vimebaki kupatiwa umeme katika Halmashauri ya Songea vijijini.
“Kijiji hicho kina wigo wa wateja 64 na kwa sasa kimeunganisha wateja 9 hivyo tunaendelea kutoa wito kwa taasisi za serikali na zisizo za serikali kutuma maombi ya kuunganishwa,” alisema Mhandisi Ndule.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Songea Ndg. Mtela Mwampamba amegusia umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya pamoja kwa familia mfuko ambao unajumuisha watu sita kutibiwa kwa mwaka mzima.
Ukiwa na bima ya afya Inasaidia kupata huduma za afya pindi magonjwa yanapojitokeza ghafla na ukiwa hauna fedha, hivyo tutumie fursa hii tuliyonayo wakati wa mavuno kujiunga na bima ya afya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho, akiwasha umeme katika kitongoji cha Shuleni kilichopo katika kijiji cha Chihurungi Halmashauri ya Songea.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho,akizungumza na wananchi wa Chihurungi na Parangu wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo.
Katibu Tawala wa wilaya ya Songea Ndg. Mtela Mwampamba akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Parangu na Chihurungi.