Chuo Cha Ufundi VETA Shinyanga kimekuja na ubunifu wa vipodozi vya matunda ya asili ambavyo havina madhara katika miili ya binadamu.
Akizungumza Leo, Julai, 5, 2024, kwenye Maonesho ya Kibiashara ya 48 ya Kimataifa ambayo yanafanyika katoka Viwanja vya Sabasaba jijini Dar-es-Salaam, Mwalimu wa Saluni,Mapambo,Urembo na Vipodozi, Judy Mwita amesema kuwa wamekuja na ubunifu huo,kwa sababu ni wa asili na hauna madhara yoyote kwa mtumiaji.
“Huu ubunifu tumeona tuje nao ili kuwapa elimu Wananchi wote ambao wanatutembelea katika banda letu,ili waweze kujifunza namna ya kutumia vitu vya asili mfano matunda,vitunguu, Abdalasini, Nazi Papai, Parachichi na vitu ambavyo ni rahisi kupatikana na visivyo na gharama kubwa ,” amesema.
Hivyo basi amewakaribisha Wananchi wote kwa ujumla kutembelea katika banda la Veta ili kujifunza na kupata elimu kuhusu namna ya matumizi ya Urembo utokanao na vitu vya asili.