Home BUSINESS BENKI YA TCB YATANGAZA FAIDA YA SH. BILIONI 19.27

BENKI YA TCB YATANGAZA FAIDA YA SH. BILIONI 19.27

Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM 

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Adam Mihayo amesema kuwa Benki hiyo imeshuhudia ongezeko kubwa la mapato ya jumla ya Shilingi Bilioni 19.27 sawa na asilimia 11.19 hadi kufika  Bilioni 19. 21, kwa mwaka 2023. ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo mapato yalikuwa Bilioni 172.83 sawa na asilimia 1.72.

Mihayo ameyasema hayo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya Benki hiyo ya mwaka 2023 katika mkutano mkuu wa 32 wa wanahisa uliofanyika leo Juni 18, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa ongezeko hilo lilichangia asilimia 79.61 ya mapato yote ya Benki, huku kiasi kilichobaki kikipatikana kutoka katika kamisheni, ada mbalimbali na shughuli nyingine zilizofanywa na Benki.

Aidha, ameongeza kuwa Taasisi hiyo ina dhamira ya dhati ya kudumisha ufanisi na kumridhisha mteja sambamba na kusikiliza na kuelewa mahitaji ya wateja wake .

Katika mkutano huo Mihayo amefafanua kwa undani mafanikio waliyoyapata mwaka 2023, na kusema kuwa Mali za  Benki hiyo ziliongezeka kutoka Shilingi Trilioni 1.285 mwishoni mwa mwaka hadi kufikia Tririon 1.389 mwishoni mwa mwaka 2023, sawa na ongezeko la asilimia 8.1 ikiwa ni sawa na Shilingi Bilioni 103. 9.

“Jumla ya mikopo yote iliongezeka kwa shilingi Bilioni 73.1 kutoka Bilioni 838 mwishoni mwa mwaka 2022 mpaka kufika Bilioni 911.2 mnamo Disemba 31, 2023 ikionyesha ongezeko la Amana za wateja ambazo ziliongezeka kwa asilimia 12.01 kutoka Trillion 1 mwishoni mwa mwaka 2022, hadi kufika Trilioni 1.12 mwishoni mwa mwaka 2023” amefafanua Mihayo.

Pia amesema, kupitia usimamizi wa kimkakati wa uwekezaji wake,  Amana za
TCB Benki katika Benki nyingine zilishuka kwa Shilingi Bilioni 55.3 (33.32%), huku Amana za Serikali zikiongezeka kwa Shilingi Bilioni 44.1 (42.64%), fedha tasilimu, ambapo salio katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT) liliongezeka kwa Shilingi Bilioni 47 sawa na asilimia 41.26.

Mbali na hayo, Mihayo amesema Benki hiyo imeboresha mifumo yake ya kibenki kwa kuanzisha mradi unaowawezesha watumiaji wa mtandao wa Tigo kutoa hela zao katika mashine za ATM za Benki hiyo.

Aidha amesema kuwa majaribio ya mashine za ATM zinazowawezesha wateja kuweka fedha zao tayari yamefanyika, ambapo huduma hiyo inatarajiwa kuzinduliwa mwaka huu.

“Tutaendelea kuhakikisha tunawawezesha kupata suluhisho la kifedha katika mahitaji yao mbalimbali, ili kuchangia katika mafanikio ya Watanzania kama ambavyo dhamira yetu ya kuwezesha ukuaji wa kiuchumi wa watu wetu inavyoeleza.”

Sambamba na hayo, Mihayo amesema Benki ilionyesha dhamira yake ya kuongeza ubunifu na kutimiza mahitaji ya wateja kwa kuzindua bidhaa zinazomlenga mteja, ambapo moja ya bidhaa hizo ni ya mikopo kwa wastaafu, (Pensioner’s Advance Loan) ambao ni mpango unaowawezesha wastaafu kupokea kiinua mgongo kabla ya wakati.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo, Martin Emmanuel Kilimba ameeleza kuwa katika kujiandaa na mwaka ujao wa fedha wanakusudia kuendelea kuboresha ufanisini wao ili kuwezesha ukuaji wa Taasisi hiyo.

“Malengo yetu ni kuendelea kuboresha mizania, kujenga taswira mpya ya taasisi yetu, kupokea teknolojia ya kidigitali, kufanya uhakiki wa hasara, na kusimamia rasilimali watu.

“Tunaamini mambo haya yatatupeleka katika kilele cha mafanikio na kutengenza thamani kwa wanahisa wetu.” ameeleza Kilimba.

Previous articleTAMKO KUHUSU HALI YA UCHUMI NA BAJETI KUU YA SERIKALI ILIYOWASILISHWA KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25
Next articleRAIS SAMIA AKIWASILI JIJINI PRETORIA AFRIKA KUSINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here