Home LOCAL KIKUNDI CHA TUNAWEZA MONGOLANDEGE UKONGA WAKABIDHIWA KATIBA, WAMPONGEZA RAIS SAMIA

KIKUNDI CHA TUNAWEZA MONGOLANDEGE UKONGA WAKABIDHIWA KATIBA, WAMPONGEZA RAIS SAMIA

 

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mongolandege, Rajabu Tego amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufungua milango kwa kutoa miongozo yenye unafuu katika usajili wa vikundi mbalimbali kisheria.

Hayo ameyasema leo Juni 16, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi katiba, kanuni na kadi ya mwanachama wa kikundi cha Tunaweza ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Mwenyekiti wa kikundi cha Tunaweza, Dk Abdallah Mandai (katikati) akizungumza wakati wa kukabidhi katiba kwĆ  wanachama, kulia ni Katibu wa kikundi hicho cha Tunaweza, Gervas Paulo, na kushoto ni katibu msaidizi Ramadhan Mtuli.

Tego amesema kuwa kuanzishwa kwa miongozo hiyo kumerahisisha usajili wa vikundi na kuondoa dhana ya kudhulimiana kutokana na fedha kukaa mifukoni mwa viongozi.

ā€œNi jambo la kumpongeza Rais Samia kuanzisha miongozo hiyo kwa vikundi vya kijamii, lakini nakipongeza kikundi cha Tunaweza ambacho kimepata usajili hivyo hata michango wanayotoa itakuwa mahala salama na kuwezesha kikundi kupata maendeleo na hata kwa mwanachama mmoja mmoja pindi inapotolewa mikopoā€ amesema.

Naye Katibu wa kikundi hicho cha Tunaweza, Gervas Paulo, amesema kuwa kikundi hicho kina wanachama 118 ambapo kilianzishwa Machi 8, 2023.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mongolandege, Jimbo la Ukonga jijini Dar ea Salaam, Rajabu Tego akikabidhi katiba kwa mwanachama wa kikundi cha Tunaweza leo Juni 16, 2024.

ā€œKikundi cha Tunaweza tayari kimepata usajili, na leo tumegawa katiba kwa wanachama ili kila mmoja afahamu sheria na kanuni tulizojiwekea ili kuepuka kwenda kinyume na taratibu za makubaliano yetuā€ amesema.

Katibu huyo amesema kuwa kikundi hiki kimeanzishwa kwa nia ya kusaidiana katika nyanja mbalimbali lakini pia katika kutoa misaada kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.

ā€œTunashirikiana katika makundi hayo na wanachama wamekuwa wakichangia ada ya sh.5,000 kwa kila mwezi na kuhifadhiwa benki ingawa bado kuna baadhi ya wanachama wako nyuma katika uchangiaji jambo ambalo wanakwenda kinyume na katiba yetu,ā€ amesema.

Ameongeza kuwa kuna mafanikio mbalimbali ambayo yamepatikana lakini pia kuna changamoto ya kuwepo kwa baadhi ya wanachama ambao si waaminifu wenye mtazamo hasi wa kuomba kupata matatizo ili wapate fedha tu hivyo tunashauri ni vyema wote tukawa wazalendo.

Naye katibu msaidizi Ramadhan Mtuli, amesema kuwa kikundi cha Tunaweza kinapokea wanachama kutoka maeneo mbalimbali ili mradi mwanachama awe na akili timamu.

ā€œTunapokea wanachama kutoka maeneo mbalimbali ili mradi awe na akili timamu hivyo tunawakaribisha wenye nia ya kutaka kujiunga na Tunaweza kwani ni kikundi kilichosajiliwa kisheria,ā€ amesema.

Hata hivyo amempongeza Rais Samia kwa kazi nzuri na kubwa anazozifanya hivyo rai yao kwake ni kuomba kuwafikia katika utaratibu wa utoaji mikopo ili wanachama waweze kunufaika na kupata maendeleo.

Baadhi ya wanachama wa kikundi cha Tunaweza wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano huo.

 

Previous articleRAIS SAMIA ASHIRIKI SALA YA EID AL ADHA JIJINI DARĀ 
Next articleMAJALIWA: WATANZANIA TUENDELEE KUDUMISHA AMANI, UPENDO NA MSHIKAMANO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here