Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Makampuni na Majina ya Biashara kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Mainrad Rweyemamu (kushoto), akikabidhi vyeti kwa baadhi ya wadau waliokamilisha tararibu za usajili wa majina ya biashara, katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa, yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. BRELA inashiriki katika maonesho hayo kwa kutoa elimu ya urasimishaji wa biashara, sambamba na usajili wa papo kwa papo.