Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka wakandarasi wazawa waliopewa dhamana ya ujenzi wa Miradi ya umwagiliji kuhakikisha waaitekelza kwa weledi na ubora wa hali ya Kuu.
Majaliwa Ameyasema hayo Jana katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa Miradi ya umwagiliaji katika maeneo mbalimbali, iliyofanyika jijini Dodoma.
“Ndugu washiriki nimefurahishwa kuona kuwa asilimia 82 ya wanaokwenda kujenga miradi hii ni wataalamu na hizi ni fursa za ajira kwa Watanzania, lakini ni fursa ya kuongeza ujuzi kupitia miradi hii, vilevile inakwenda kuongeza kipato kwa Watanzania.
“Nitoke rai kwa wakandarasi wazawa, kwanza mbadilike, mnathaani kubwa mmepewa ya kutekeleza miradi na hili ndicho kilio kikubwa cha private seckta (sekta binafsi) leo mmeona serikali imeendelea kutekeleza kwa kuwapa miradi.
“Mjipange vizuri tumieni fursa hii kuihakikishia serikali kwamba mnaweza, lakini nyie mna dhamira zenu kufungua kampuni za ukenzi, mna hiyo dhamira simamieni dhamira zenu. Sisi tunakutegemeeni nyie kufua milango ya ajira