Home LOCAL JET YAWANOA WAHARIRI

JET YAWANOA WAHARIRI

Na: Jimmy Kiango, BAGAMOYO

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET), kimefanya semina ya siku tatu na wahariri zaidi ya 20 Bagamoyo, mkoani Pwani kwa ajili ya kuwaongezea uwezo  juu ya utunzaji wa mazingira na namna ya kukabiliana na biashara haramu ya Wanyama pori.

Semina hiyo ambayo ilianza Julai 7, 2022 pia ilihusisha wadau mbalimbali wa mazingira likiwemo shirika la TRAFFIC ambalo linajihusisha na mapambano dhidi ya biashara haramu ya Wanyama pori pamoja na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID).

Dhamira kuu ya semina hiyo ni kuwajumuisha wahariri katika mapambano dhidi ya ujangili na uharibifu wa mazingira.

Akizungumza na wahariri kwenye ufunguzi wa semina hiyo mwakilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Raphael Manirabarusha, alisema ni jukumu la wahariri wa nchi za Afrika Mashariki kuhakikisha wanashiriki kwenye kuielemisha jamii juu ya utunzani wa mazingira.

“Tunapaswa kukubaliana kuwa jukumu la utunzaji wa mazingira ni letu sote, lakini ninyi wahariri kwa kutumia kalamu zenu, mnalo jukumu kubwa la kushiriki kwenye suala hili la utunzaji wa mazingira kwa sababu ninyi mnafikisha ujumbe kwa haraka,”alisema Manirabarusha.

Nae mwakilishi wa TRAFFIC, Jane Shuma alisema ushirikiano uliopo kati ya taasisi yao na JET utasaidia kwa kiasi kikubwa kufikisha kwa haraka taarifa zinazohusu mapambano yao dhidi ya biashara haramu ya wanyamapori.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa JET, John Chikomo alisema anaamini semina hiyo itakuwa na faida kubwa kwa nchi kwani hatua ya wahariri kuwa na ufahamu mkubwa juu ya utunzaji wa mazingira, itasaidia kuikomboa nchi na uharibifu wa mazingira na masuala ya ujangili.

MWISHO..

Previous articleTCU YATANGAZA KUFUNGUA DIRISHA LA UDAHILI KWA WAOMBAJI WA SHAHADA YA KWANZA KUANZIA LEO JULAI 8 HADI 15, 2022
Next articleMATUMIZI SAHIHI YA RASILIMALI YA MAJI YNAHITAJIKA KUKABILINA NA CHANGAMOTO YA MAJI KWENYE KILIMO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here