Home LOCAL MADEREVA BODA BODA WASIMULIA WALIVYONUFAIKA NA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI

MADEREVA BODA BODA WASIMULIA WALIVYONUFAIKA NA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI

DodomaNa: Mean Wetu-DODOMA

MADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya elimu ya usalama barabarani yalivyo wafumbua macho na kuwafanya kufahamu sheria mbalimbali za barabarani na hivyo kuendelea na kazi yao wakiwa salama.

Wamesema hayo mbele ya waandishi wa habari waliokuwa wametembelea kijiwe cha bodaboda cha Kijiwe Pesa ambapo baadhi ya bodaboda walikuwa wakifanya tathimini kuhusu mafunzo waliyopata kutoka Amend kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uswisi ambao wameendelea kufanikisha kutolewa kwa mafunzo hayo.

Madereva hao bodaboda katika kijiwe hicho wamesema awali hawakuwa wakifahamu vema sheria za usalama barabarani hasa taa zinazoongoza magari na jinsi ya kupita kwenye makutano ya barabara ilikuwa ni kitendawili kwao.

“Kupitia mafunzo ya usalama barabarani ambayo tumeyapata kutoka kwa wenzetu wa Amend kwa kushirikiana na wadau wengine kama Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani sasa tunafahamu vema sheria za usalama barabarani pamoja na alama zilizopo,” amesema dereva bodaboda
Jonathan Chidawi

Kwa upande wake Amiri Matimba ambaye ni Msaidizi wa Miradi kutoka Shirika la Amend Tanzania anasema wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa madereva bodaboda 47 kwa wiki ya kwanza jijini Dodoma.

Ameongeza kuwa wanaendelea kutembea katika vijiwe mbalimbali vya bodaboda kwa ajili ya kuhamasisha maofisa hao kusafirishaji (bodaboda) kujiunga katika mafunzo hayo yanayotolewa bila gharama yoyote.

Wakati huo huo Mkufunzi wa Mafunzo hayo ambae pia ni Katibu wa Chama cha Walimu wa madereva Tanzania (CHAWATA) Massava Ponera akieleza tathimi ya mafunzo hayo toka walipoanza hadi walipofikia amesema mafunzo yanaendelea na madereva wengi wamefikiwa na mafunzo hayo.

Amefafanua kwa Dodoma hiyo ni awamu ya pili kutolewa kwa mafunzo hayo ambayo yamedhaminiwa na ubalozi wa Uswisi ili kuwezesha elimu ya usalama barabarani inafika kwa kundi la bodaboda ambalo jamii siku zote hulitazama kwa jicho la tofauti na kuamini ni wavunjaji wa sheria wakubwa.

Mwisho.

Previous articleEMPOWERING FEMALE ENTREPRENEURS AND BUSINESS OWNERS: CFAO MOBILITY TANZANIA AND STANBIC BIASHARA INCUBATOR UNITE ON INTERNATIONAL WOMEN’S DAY
Next articleBAJETI YA MATENGENEZO MIUNDOMBINU YA UMEME KUENDELEA KUONGEZWA KILA MWAKA- MHE.KAPINGA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

1 COMMENT

  1. Exclusive B2B Lead Generation Services at Competitive Prices

    Dear,

    I hope this message finds you well.

    We specialize in offering exclusive B2B lead generation services tailored to help businesses like yours thrive.
    With our strategic approach, you can expect high-quality leads that drive growth—all at competitive prices.

    We would love to discuss how we can support your business goals with our affordable, results-driven services.
    Please feel free to reach out, and let’s explore how we can collaborate for your success.

    Simply Visit us on Fiverr @ https://bit.ly/3ZwIxoi

    Looking forward to hearing from you.

    Best regards,

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here