NA: HERI SHABAN ILALA, herishaban@gmail.com
SERIKALI inatarajia kufanya tathimini upya kwa ajili ya kulipa fidia kwa Wakazi zaidi ya 2000 wa Mtaa wa Kipunguni kata ya Kipawa Wilayani llala kwa ajili ya kupisha upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Tamko hilo la Serikali lilitolewa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Atupele Mwakibete ambapo mara baada upanuzi huo Wananchi hao watakumbwa na Bomoa Bomoa kwa ajili ya kupisha upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.
Naibu Waziri Mwakibete alisema tathimini hiyo ya Wakazi wa Kipunguni inatarajia kufanyika Julai 14/2022 mwaka huu kwa Wakazi wote wa Mtaa wa Kipunguni ambao walisitisha kuendeleza maeneo yao toka mwaka 1997.
“Serikali umetenga fedha za kuwalipa itafanyika tathimini ya Sasa sio ya zamani kila mtu atalipwa pesa zake ili kufanikisha malengo ya Serikali katika upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere” alisema Mwakibete
Naibu Waziri Mwakibete aliwataka wakazi wa Mtaa Kipunguni kuwapa ushirikiano Wataalam wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA )watafanya tathimini na Wataalam wa Serikali katika zoezi hilo.
Alisema zoezi hilo la kufanya tathimi kwa wakazi wa Kipunguni linatarajia kumalizika October mwaka huu ndio waanze kulipwa pesa zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege TAA Mussa Mbula, alisema fungu lipo kwa ajili ya malipo ya fidia ya Sasa kwa ajili ya kuwalipa Wananchi wa eneo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli, alisema wakazi wake wa Kipunguni Kata ya Kipawa toka mwaka 1997 walisitisha ujenzi kuendeleza maeneo yao Sasa ufumbuzi wake umepatikana serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekubali kufanya tathimini upya kwa Sheria za sasa kwa ajili ya kutathimini ardhi upya na wote watalipwa.
Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli alisema wakazi wake wa KIPUNGUNI kata ya Kipawa zaidi ya miaka 25 wameshindwa kuendeleza maeneo yao na kukosa mikopo mikubwa badaa serikali kuwataka wapishe maeneo yao kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.
“Katika vipindi vyangu vya Uongozi nikiwa Mbunge wa Jimbo la Segerea nimewapambania Wananchi wangu nikiwa Bungeni kuwatetea waweze kufanyiwa tathimini upya waweze kulipwa nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kilio cha Wananchi wangu kimepata ufumbuzi wake wote watalipwa na Serikali yetu sikivu ” alisema Mbunge Bonah.
Diwani wa Kata ya Kipawa Aidan Kwezi ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi na Mbunge wa Jimbo la Segerea Katika kupatia ufumbuzi wake wakazi wa Mtaa wa Kipunguni.
Mwisho