Home BUSINESS MIAKA 3 YA Dkt. SAMIA, TANAPA WAONGEZA MAPATO, SEKTA YA UTALII...

MIAKA 3 YA Dkt. SAMIA, TANAPA WAONGEZA MAPATO, SEKTA YA UTALII YAIMARIKA

Kamishna wa Uhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Juma Kuji, akizungumza alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu mafanikio ya Shirika hilo kwenye mkutano na Wahariri wa Habari uliofanyika leo Machi 21, 2024 Jijini Dar es Salaam, chini ya Uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Sabatho Kosuri Afisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, akiongoza mjadala na maswali, maswali na michango mbalimbali kutoka kwa Wahariri na waandishi wa Habari katika mkutano huo.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Deodaus Balile, akizungumza kwaniaba ya Wahariri, katika mkutano huo.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Anitha Mendoza katika mkutano huo.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM 

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), limefanikiwa kuongeza mapato katika kipindi cha miaka mitatu kutoka shilingi 174,715,158,494 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 hadi kufikia shilingi 337,424,076,896 kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Akizungumza leo Machi 21, 2024 Jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Kamishna wa Uhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Juma Kuji, amesema kuwa kuna ongezeko la mapato la shilingi162,708, 918,402 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 94.

Kamishna Kuji amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 kuanzia mwezi Julai 2023 hadi Machi 19, 2024 TANAPA imefanikiwa kukusanya shilingi 340,101,108,465 ukilinganisha na matarajio ya kukusanya shilingi 295,466,811, 506 mpaka Machi 2024.

Amefafanua kuwa mapato ya sasa yanazidi mapato ya shilingi 282,450,446,103 yaliyokusanywa mwaka 2018/2019 kabla ya janga la UVIKO – 19 ambayo yalikuwa ndio kiwango cha juu cha mapato katika Shirika hilo.

“Kuna ongezeko la watalii na mapato ambayo yanakwenda pamoja na malengo ya Ilani ya Chama Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2020 – 2025 inayoelekeza idadi ya watalii nchini kufikia milioni 5 na mapato ya dola za kimarekani Bilioni 6 kwa mwaka ifikapo mwaka 2025” amesema Kamishna Kuji.

Amebainisha kuwa pia idadi ya watalii nchini imeongezeka kutoka watalii 997, 873 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 hadi kufikia 1,670,437 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Amesema kuwa kwa mwaka huu wa fedha 2023/2024 kuanzia Julai 2023 hadi Machi 19, 2024 idadi ya watalii walikuwa 1,514,726.

Kamishna Kuji amesema kuwa watalii wa ndani ni 721,543 uku watalii kutoka Mataifa mbalimbali wakiwa 793,183.

Amefafanua kuwa watalii waliotembelea Hifadhi za Taifa sawa na ongezeko la asilimia 5 ikiwa ni zaidi ya lengo la kupokea watalii 1,387,987 (wa nje 827,713 na watalii wa ndani 726,676) katika kipindi husika.

Amesema kuwa idadi ya watalii wanaotarajiwa kutembelea Hifadhi za Taifa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ni 1,830,081 (watalii wa nje 963,413 na watalii wa ndani 866,667).

“Kipindi cha miaka mitatu kumekuwepo na ongezeko la siku za kukaa wageni kutoka wastani wa siku 1,749,194 katika mwaka wa fedha 2021/2022 hadi kufikia wastani wa siku 2,669,586 kufikia Februari 2024” amesema Kamishna Kuji.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Makamu wa Rais wa Jukwaa la Wahariri Afrika Mashariki Bw. Bw. Deodatus Balile ameitaka TANAPA kuvitumia vyombo vya habari katika kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji.

Bw. Balile amesema kuwa wakati umefika kwa TANAPA kutumia fursa mbalimbali kwa kubadilisha Sheria au kutumia kanuni ili kuhifdhi maziko ya viongozi wa Taifa na kuwa sehemu ya hifadhi kama ilivyo kwa nchi nyengine.

Previous articleSOMA HABARI MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MACHI 21-2024
Next articleWATU 1404 WAKUMBWA NA MAFURIKO KILOSA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here