Home LOCAL PPRA YAWAPIGA ‘MSASA’ WATUMISHI WA MSD KUHUSU MFUMO MPYA WA UNUNUZI WA...

PPRA YAWAPIGA ‘MSASA’ WATUMISHI WA MSD KUHUSU MFUMO MPYA WA UNUNUZI WA UMMA KWA NJIA YA MTANDAO (NeST)

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Mavere Tukai amesema watumishi wa MSD wanapaswa kushiriki na kujifunza kikamilifu mfumo huu ili kuhakikisha mfumo unatatua changamoto mbalimbali za kiutendaji na kuleta tija katika upatikanaji wa bidhaa za afya nchini.

“ MSD tumewekeza sehemu kubwa katika kuhakikisha mfumo huu unakuwa na tija katika manunuzi ya bidhaa za afya. Tuna timu ambayo inafanyakazi na timu ya kitaifa inayotengeneza mfumo huu ili kuhakikisha unawezesha kwa ufasaha majukumu ya MSD”. Amesema Tukai.

Naye mkufunzi kutoka Mamlaka ya udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Bw. Castor Claudius Komba – Meneja Mafunzo na Ushauri amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha watumishi wa MSD wanakuwa na uelewa wa hali ya juu katika matumizi ya mfumo huo, kwani MSD ina majukumu nyeti ya kununua bidhaa za afya hivyo mfumo huu haupaswi kuwa kikwazo katika manunuzi ya bidhaa za afya nchini.

Pia Bw. Komba ameongeza kuwa anatarajia kuwa mfumo huo mpya utatatua changamoto zilizokuwepo wakati wa matumizi ya mfumo wa ununuzi wa Taneps.

Mafunzo haya ya Mfumo mpya wa Ununuzi wa Umma kwa Njia ya Mtandao (NeST) yanatolewa kwa siku tano kwa watumishi wa MSD wanaotoka Makao Makuu na Kanda za MSD.

Previous articleRAIS SAMIA KUONGOZA MAZISHI YA LOWASSA FEBR. 17
Next articleJUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF) WAMLILIA LOWASA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Open chat
GREEN WAVES MEDIA
Ahsante kwa kutembeiea PPRA YAWAPIGA ‘MSASA’ WATUMISHI WA MSD KUHUSU MFUMO MPYA WA UNUNUZI WA UMMA KWA NJIA YA MTANDAO (NeST)