Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Maaluum ya Wasioona Buigiri wakifurahia jambo wakati Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi.Jenifa Christian Omolo alipowakabidhi kadi 100 za bima ya afya za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya, mkoani Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi.Jenifa Christian Omolo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Maaluum ya Wasioona Buigiri, Bw. Samwel Jonathan wakimkabishi Mwanafunzi wa Darasa la Awali wa Shule hiyo, Zulfat Ibrahimu, kadi ya bima ya afya za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Dodoma. Wakishuhudiwa na wawakilishi wa viongozi na wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi TUGHE tawi la Wizara hiyo, Bi. Hilda Segele, Bi. Scholastica Okudo, Bi. Halima Juma, Bi. Mariam Kiangi na Mwalimu wa Shule hiyo, Wakati Joseph.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi.Jenifa Christian Omolo, akiwa katika picha na wanafunzi wa Shule ya Msingi Maaluum ya Wasioona Buigiri, iliyopo Chamwino mkoani Dodoma, baada ya kuwakabidhi kadi 100 za bima ya afya za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kurahisisha matibabu.
Â
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)