BAADHI ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wakishiriki ujenzi wa Taifa katika mradi huo wa kitega uchumi wa UVCCM Mkoa wa Kaskazini Pemba.
–Mkuu wa Matembezi Mhe.Machano Ali Machano,akiwahamasisha Vijana wa Matembezi mara baada ya kuwasili Wilaya ya Wete Pemba.
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe.Salama Mbarouk Khaib akizungumza na Vijana wa Chama Cha Mapinduzi waliopo katika Matembezi mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Wete Pemba kwa ajili ya kufanya ujenzi wa Taifa katika mradi wa jengo la kitega uchumi cha UVCCM Mkoa huo.
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema kupitia maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi imetekeleza miradi ya kimkakati yenye dhamira ya kukabili changamoto ya mfumko wa bei za vyakula baada ya kukamilika kwa ujenzi wa ghala kubwa la kuhifadhia chakula katika bandari ya wete mkoa wa Kaskazini pemba.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkao wa Kaskazini Pemba Mhe.Salama Mborouk Khatib,wakati akizungum na vijana wa Matembezi ya UVCCM ya kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ujenzi wa Taifa wa mradi wa nyumba ya kitega uchumi cha UVCCM Mkoa huo.
Mhe.Salama ,amesema ghala hilo limejengwa  na kampuni ya Yassin provision store lenye uwezo wa kubeba tani 8,000 za vyakula na litasaidia kupunguza bei za vyakula kwa upande wa kisiwani Pemba ambapo vyakula vya aina zote vinatarajiwa kuingizwa kutoka nchi jirani kama vile Kenya, Rwanda,Burundi na nchi nyengine za jirani ambapo amesema bei ya mchele
itapungua sana hususan kwa bei ya jumlaa kwa wafanya biashara wakubwa kisiwani pemba.
Amesema miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar kwenye mkoa wake wa kaskazini Pemba  jumla ya miradi 5 mikubwa imetekelezwa kwa ufanisi mkubwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
chini ya Rais dk Hussein Ali Mwinyi ambapo skuli za Ghorofa saba na mbili zimekamilika na tano zipo katika hatua ya mwisho ya kukamilika .
Akizungumzia mradi wa maji safi na salama tayari umekamilika sambamba na ujenzi wa miundombinu ya barabara za ndani.
Katika maelezo yake Mhe.Salama alisema Serikali imetoa fursa za uwezeshaji wa makundi mbalimbali ya Vijana ili wajiajiri na kujiongezea kipato.
Pamoja na hao alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejenga masoko mawili makubwa katika eneo la kivumbi kai na Tumbe wilaya ya micheweni ambapo kila soko limegharimu kiasi cha Shilingi bilioni 1.5.
Nae Mkuu wa Matembezi hayo Mhe.Machano Ali Machano ,amesema miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar inaakiwa kuenziwa kwa vitendo kwa kuanzisha miradi ya maendeleo itakayowanufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum kupiia kundi la Vijana Mkoa wa Katavi Mhe.Lucy… amepongeza jitihada za vijana kwa upande wa kaskazini pemba kwa kuanzisha miradi ambayo imewezesha kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndugu Hashir Ali Said,alisema mradi huo wa jengo lenye ghorofa tatu utagharimu kiasi cha shilingi milioni 470 unaojengwa katika eneo la Wilaya ya Wete.
Mradi huo ndio uliohiimisha maembezi hayo kwa upande wa Pemba na yataendelea Tarehe Januari 1,mwaka 2024 katika Mkoa wa Kusini Unguja.