TIMU ya Biashara United ya Mara, kinatarajia kuondoka kesho nchini kuelekea Djibout kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya wenyeji wao, FC Dikhil ya Djibout katika michezo ya hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).
Hata hivyo Biashara United ikiwa ni mara ya kwanza kushiriki michuani hiyo na itaanzia ugenini dhidi ya F C Dikhil, mchezo utakaopigwa Septemba 10, mwaka huu nchini humo.
Kauli hiyo imetolewa na Kocha Mkuu Patrick Odhiambo,wakati wakiwa mazoezi leo anasema ana imani kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo wa ugenini baada ya kuona ubora na mapungufu ya wapinzani wao wanapokuwa kwenye nyumbani.Anasema kwa kuwaangalia wapinzani wao hao na maamdalizi waliyoyafanya kwenye Pre Season, ana matarajio makubwa ya kufanya vizuri na kurejea na matokeo chanja.
“Tuko sawa, tumefanya maandalizi ya kutosha licha ya kutopata mechi za kirafiki za kimataifa ila tumecheza na timu za nyumbani na kupata mazoezi makubwa, kuwepo kwa wachezaji wa kimataifa wenye uzoefu wa michuano itawasaidia kupata matokeo katika mechi yetu hiyo,” anasema Odhiambo.
Anasema uwepo wa nyota hao ni Ramadhani Ridondo ‘Chombo’ aliyewahi kupita Simba, wengine ni kutoka nje ya Tanzania ambao ni Baron okech onyango, Opare collins na Odongo.
Ameongeza kuwa wanaenda kwenye michuano hiyo kuiwakilisha Tanzania na sio Biashara United pekee, kuhakikisha wachezaji wake wanapambana kupata matokeo mazuri katika mechi zote kwa lengo la kuendele kusonga mbele na kuitunza nafasi ya timu nne kwa taifa kushiriki michuano ya Kiamtaifa.
Anaongeza kuwa katika mchezo huo watawakosa nyota wao watatu akiwemo nahodha mkuu, Abdulmajid Mangalo ambaye jina lake haliko katika orodha ya majina ya wachezaji waliopelekwa CAF kutokana na kuchelewa kujiunga ndani ya kikodi cha timu hiyo.
Naye Chombo amesema wamejipanga vizuri na wanaenda kupamban kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.