Na Mwandishi wetu
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TCAA) imepokea kontena 9 zenye mitambo kwa ajili ya kuboresha mawasiliano kati ya waongoza ndege na rubani na vifaa vya kurefusha na kukuza sauti vinaenda kufungwa katika vituo 18 nchi nzima.
Akizungumza leo Oktoba 27 na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kupokea kontena hizo Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema serikali iiietenga bilioni 31.5 kwa ajili ya kuboresha mawasiliano katika viwanja vya ndege nchini huku lengo ni kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa viwanja vya ndege na wigo wa usafiri wa anga.
“Nimpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga kiasi cha bilion 31.5 kwa ajili ya kuboresha mifumo ya mawasiliano kwenye viwanja vya ndege kati ya waongoza ndege na rubani,”amesema Johari.
Amesema baada ya serikali kutoa fedha walitangaza zabuni shindanishi za kimataifa na kupatikana mzabuni kutoka nchi za Norway na Italy ambae ameshinda na ndio aliyeleta kontena hizo za mitambo hiyo.
Amesema wakiwa wanajiandaa na maboresho hayo TCAA iliwapeleka wataalam wake 24 nchini Italy na Norway kwa ajili ya kupata mafunzo ya mitambo hiyo.
Johari ametaja maeneo ambayo vituo ambayo vitafungwa mitambo hiyo ni pamoja na Uwanja wa Ndege cha kimataifa Julius nyerere,Uwanja Abed Amani Karume Zanzibar, Songwe, Pemba Mwanza,Tabora,Kigoma,Dodoma Mtwara,Tanga,Kilimanjaro na Arusha.
Amesema baada ya kufungwa mitambo hiyo kwenye viwanja hivyo pia kutakua na vituo vya kurefusha na kukuza mawasiliano ya sauti ambavyo vituo hivyo vitakua 18 nchi nzima.
Ametaja vituo hivyo ambavyo ni Matogoro, Kiuwe, Songea,Mbunga Mtwara,Mwasenyi ,Rufiji,Michakani Pemba, Arusha,bOldeianamalanja, Ngorongoro, Kwejunga Tanga, Gairo Morogoro, Dodoma, Mwisi Tabora,kigoma,Nyamanya Bihalamuro,Mbiso Katavi,Kitulo,Muganza Butiama,Mara na Mugumu.
“Tunachotarajia baada ya kufunga mitambo hii ni mawasiliano kati ya marubani na waongoza ndege katika anga lote la Tanzania na anga la juu la nchi ya Burundi yatakuwa yameborehwa kwa mujibu wa viwango vya kimataifa,”amesema Johari
Ameongeza baada ya kufungwa mitambo hiyo huduma za usafiri wa anga zitaimarika maradufu na kuchagiza idadi ya miruko ya ndege katika nchi na idadi ya mashirika ya ndege yanayokuja nchini lakini pia idadi ya abiria na kusapoti royal tour kwa kupata idadi kubwa ya watalii.
Aidha mitambo iliyopokelewa ni radio za kidigital za masafa ya juu inayojulikana Kama VHF,mitambo ya kurekodi mifumo ya mawasiliano ya sauti(digital voice recording system) pamoja na mifumo ya kuunganisha ya kuangalia mawasiliano.
Kwa upande wake Mkurugenzi Huduma za Uongozaji Ndege TCAA, Frola Mwanshinga amesema kufungwa kwa mitambo hiyo kutaboresha huduma na kuongeza idadi ya kampuni za ndege nchini na wanategemea mifumo yao kuwa sambamba na mifumo ya nchi nyingine jirani na kuweza kufanyakazi kwa pamoja.