NA: HERI SHAABAN.
MKUU wa Wilaya Ilala Ng ‘wilabuzu Ludigija ametatua mgogoro wa ARDHI Kifuru kata ya Kinyerezi Wilayani Ilala kwa kuagiza Maafisa ARDHI kuhakiki upya eneo hilo na kumaliza changamoto iliyokuwepo zaidi ya miaka kumi.
Akizungumza katika kikao cha wananchi Mtaa wa Kifuru Kata ya Kinyerezi Wilaya Ilala Arch, Ludigija alisema kuanzia jumatatu Maafisa ARDHI watahakiki upya eneo na kila mtu atabaki na eneo lake ambalo anamiliki bila kuwekewa vikwazo.
Arch ,Ludigija aliwataka wakazi wa Kinyerezi wakiuza maeneo ya ardhi wafuate michoro ya ramani na kujiepusha na mgogoro ya mara kwa mara
Aliwataka wananchi wa Wilaya Ilala wanaponunua ardhi au Mali yoyote wawashirikishe wake zao kwa ajili ya kuja kuwasaidia.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya aliongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ,Tabu Shaibu ,Maafisa Ardhi,Wanasheria ,Wataalam mbalimbali na wanasheri.
Kwa upande wake Diwani wa Kinyerezi Leah Mgitu ametoa kilio chake Serikali kuhusiana na msitu wa Nyuki kwa sasa imekuwa kichaka watu wanatupwa katika pori hilo sio msitu wa nyuki hivyo ameomba Serikali kulichukua poli hilo walisafishe libadilishwe matumizi litumike kwa huduma za jamii
Diwani Leah ameomba Serikali kuchukua hatua za haraka kulipatia ufumbuzi suala la msitu huo wa nyuki ambalo linahatarisha usalama wa watu na Mali na makazi.
Leah alitaka wananchi wake na Wapiga kura wa Kinyerezi wasisumbuliwe ajalizishwa na kitendo cha Kufungwa kwa akaunti ya mradi wa kurasimisha makazi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salam Tabu Shaibu amemsimamisha Mkandarasi wa Taka Kata Kinyerezi kwa kukosa sifa ya kazi hiyo akidaiwa kulalamikiwa na wanachi kutokana na huduma yake anayotoa .
Mwisho..