Tanga.
Uongozi wa Hospital ya Tanga jiji umeishukuru serikali kupitia MSD kwa kuendelea kuwapatia dawa na vifaa tiba kwa wakati jambo ambalo limeongeza tija katika utoaji huduma za afya kwenye hospitali hiyo.
Akizumgumza mara baada ya kupokea vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi millioni 250 Dkt. Rashid Said Seleman ambaye ni Mganga mfawidhi Hospital ya Jiji la Tanga amesema kuwa wana mshukuru Mhe.Rais Dkt.Samia Sulubu Hassani, kwa kuendelea kuboresha huduma za afya nchini.
“Siku ya leo tumeletewa vifaa mbalimbali kama vile vitanda,magodoro, na vifaa tiba mbalimbali ambavyo vinatusaidia kutoa huduma katika hospital yetu ya jiji la Tanga kwani ukizingatia hospital hii ni mpya lakini kwa kiasi kikubwa imeendelea kupokea vifaa mbalimbali kutoka MSD na hivyo kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.”
Aidha, ameipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa utayari wake katika kuwahudumia huku, akisifu mabadiliko chanya ya huduma yaliyoanza kuonekana
“Kwakweli tunaishukuru MSD kwani wamekuwa na ushirikiano mkubwa pia pale ambapo tuna hitaji dawa au vifaa tiba, kwakweli kuna mabadiliko makubwa ya utoaji wa huduma tofauti na hapo awali, kwani kwasasa tunaona kunaongezeko kubwa la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kutoka MSD.” Alisema
Kwa upande wake Bi. Mary Clement Afisa huduma kwa wateja wa MSD Kanda ya Tanga, alisema kuwa katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja wao kama Bohari ya Dawa hapa nchini wanaendelea kuwahudumia wateja wao, na hivyo kuziomba hospital zote kuendelea kutuma mahitaji yao na MSD itaendelea kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinawafikia kwa wakati.