Home BUSINESS Dkt. KAYANDABILA: MALENGO YA BoT NI KUNUNUA TANI 6 ZA DHAHABU KWA...

Dkt. KAYANDABILA: MALENGO YA BoT NI KUNUNUA TANI 6 ZA DHAHABU KWA MWAKA

:Naibu Gavana wa BoT, Dkt. Yamungu Kayandabila Akizungumza katika semina kuhusu fursa zilizopo kwenye mnyororo wa thamani katika sekta ya Madini hasa watoa huduma kwenye migodi, ukumbi wa Mkapa kwenye Maonesho ya Teknolojia ya Madini, Viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita Septemba 28, 2023.

Meneja Msaidizi, Upatikanaji na Usimamizi wa akiba ya Fedha za kigeni nchini BoT Dkt. Anna LyimoLyimo akifafanua mambo mbalimbali katika semina hiyo iliyofanyika mjini Geita Septemba 28, 2023.

Naibu Gavana wa BoT, Dkt. Yamungu Kayandabila akiwa katika semina hiyo na watenaji na viongozi wengine katika sekta ya madini.

Meneja Msaidizi, Upatikanaji na Usimamizi wa akiba ya Fedha za kigeni nchini BoT Dkt. Anna Lyimo akijadiliana jambo na Mkurugezi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa STAMICO Dkt. Venance Mwase mara banda ya kumalizika kwa semina hiyo iliyofanyika mjini Geita Septemba 28, 2023.

GEITA 

Naibu Gavana Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Yamungu Kayandabila, amesema kuwa Benki hiyo imejipanga kununua  tani sita za Dhahabu kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa ajili ya kuweka akiba katika mfumo wa fedha za kigeni.

Dkt. Kayandabila ameyasema hayo katika semina iliyohusu fursa zilizopo kwenye mnyororo wa thamani katika sekta ya Madini husuani kwa watoa huduma kwenye migodi, iliyofanyika Septemba 28, 2023 katika ukumbi wa Mkapa  kwenye  Maonesho ya Teknolojia ya Madini, Viwanja vya EPZ Bombambili mjini Geita.

Amesema kuwa Benki hiyo tayari imeanza kutekeleza utaratibu huo baada Bodi ya Wakurugenzi kutoa maelekezo ya kununua dhahabu kwa lengo la kuleta tija kwa Taifa.

Aidha, amesema kuwa utaratibu wa kununua dhahabu na kuihifadhi katika mfumo wa fedha za kigeni siyo mpya kwani uliwai kutumika mwaka 1990.

“Tunaifadhi fedha za kigeni kupitia dhahabu kwa kuzingatia sheria katika utekelezaji wa majukumu yetu,” Amesema Dkt. Kayandabila.

Naye Meneja Msaidizi, Upatikanaji na Usimamizi wa akiba ya Fedha za kigeni nchini BoT Dkt. Anna Lyimo, amesema kuwa mpaka sasa tayari BoT imenunua kilo 418 za dhahabu kutoka kwa wachimbaji wadogo na wa kubwa kwenda kuhifadhi katika mfumo wa fedha za kigeni.

Dkt. Lyimo amesema kuwa baada ya kununua dhahabu wataipitisha katika Viwanda vya kuchenjua vilivyopo nchini kwa ajili ya kuongeza thamani na kupunguza kuwa na mzigo mkubwa wa kusafirisha kwenda kuhifadhi.

Amefafanua kuwa baada ya kuchenjua dhahabu watazipeleka katika viwanda vya nje ya nchi kwa ajili ya kuthibitisha ubora kabla ya kuhifadhi.

“Tunakwenda kuthibitisha ubora kutokana na kwamba dhahabu inatakiwa itunzwe ikiwa na ubora wa asilimia 99. 5 hadi 99.9 ili kukidhii vigezo vya kuweka akiba katika mfumo wa fedha za kigeni” amesema Dkt. Lyimo.

Dkt. Lyimo amesema kuwa watatumia bei ya soko la dunia katika kununua, huku akieleza kuwa muuzaji wa dhahabu anapaswa kuwa na leseni kutoka Tume ya Madini.

“Bei ya Soko ya Dunia itamuongezea faida zaidi muuzaji kwani itakuwa imempunguzia gharama za uendeshaji na ndani ya saa 48 atapata fedha yake ambapo atalipwa kwa fedha ya Tanzania” amesema Dkt. Lyimo.

Ameongeza kuwa tayari wameingia makubaliano na viwanda vya kuchenjua dhahabu na kutengeneza mnyonyoro wa thamani kwa ufanisi ili kufikia malengo tarajiwa.

“Tayari tumepata wauzaji wa dhahabu 45 na baadhi tayari wamesaini mkataba kwa ajili ya kuanza manunuzi” amesema
Dkt. Lyimo

Previous articleRAIS Dkt. MWINYI ANA NIA YA DHATI YA KULETA MAENDELEO VISIWANI ZANZIBAR – COMRED MBETTO
Next articleUGANDA WAJIFUNZA TEKNOLOJIA MADINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here