Home LOCAL TEF YATEUA KIKOSI KAZI KUONGEZA NGUVU MABADILIKO YA SHERIA ZA HABARI

TEF YATEUA KIKOSI KAZI KUONGEZA NGUVU MABADILIKO YA SHERIA ZA HABARI

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limefanya kikao na wanataaluma washauri (mentors) wa habari kwa ajili ya kusimamia waandishi wa habari zinazohusu mabadiliko ya sheria za habari nchini.

Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, kimefanyika tarehe 15 Julai 2022 katika Ofisi ya TEF, jijini Dar es Salaam.

Wanataaluma walioteuliwa kusimamia waandishi ni Joseph Kulangwa, Mhariri wa Raia Mwema; Stella Aron, Mhariri wa Majira; Rashidi Kejo, Mhariri wa Mwananchi; Angela Akilimali, Mhariri wa TBC; Joe Nakajumo na Midladjy Maez; Wahariri Wastaafu.

Angela Mang’enya amepangwa kuwakufunzi Fatma Hassan Ali (Channel Ten), Kissa Daniel (East Africa Tv), Faridy Mohammed (Mlimani Tv), Godfrey Monyo (ITV).

Joseph Nakajumo atawasimamia Christopher James (Radio One), Salma Juma (Classic Fm), Philip Nyiti (Clouds Media) na Brumo Bomola (Radio Tumaini).

Rashid Kejo atakuwa na waandishi Regina Mkonde (Mwanahalisi Online), Faraja Masinde (Mtanzania Digital), Brighter Davidi (Daily News Digital) na Iddy Lugendo wa Majira.

Joseph Kulangwa amepangiwa Alex Kazenga (Jamhuri Media), Peter Elias (Mwananchi), Mery Geofrey (Nipashe) na Goodluck Hongo wa Tanzania Daima.

Srella Aron atasimamia Anneth Nyoni (Tumaini TV), Humphrey Msechu (Spatklight TV), Jackline Martin (Times Majira) na Yusuph Digossi (IBN TV).

Kwenye timu hiyo, Maez atakuwa na kazi ya kupitia kazi na kuandika ripoti.

Previous articleSINGIDA VETERAN WAADHIMISHA SIKU YAO KWA MICHEZO NA KUHAMASISHA SENSA
Next articleSERIKALI IMEJIPANGA KUENDELEZA MIRADI MBALIMBALI KATIKA SEKTA YA MADINI HAPA NCHINI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here