Ni Bi Silvester Lemburis mkazi wa Kijiji Cha Oldonyowas akielezea namna shule hiyo ilivyowasaidia kuondokana na mimba mashuleni
|
NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Taasisi ya sekta binafsi Tanzania(TPSF) kwa kushirikiana na wizara ya maliasili na utalii pamoja na mdau wa maendeleo Trade mark East Afrika kupitia mradi mkubwa wa Biashara salama wamekutana jijini Arusha kuwajengea uwezo waadau wa sekta binafsi wa kuweza kupona kiuchumi.
Mkurugenzi wa huduma kwa wanachama,uwezeshaji na kuwafikia wadau Bwn.Zachy Mbenna amesema lengo ni kuwapa uwezo wa kufungua na kujua fursa nyingi ambazo zimejitokeza kutokana na COVID.
Amesema kuwa kufuatia tafiti zilizofanywa Tanzania na zilizofanywa katika ukanda wa Afrika Mashariki zimeonyesha kwamba sekta ya utalii imeathirika kwa kiwango kikubwa na ugonjwa wa COVID -19 huku baadhi ya sekta hizo zikiathirika kwa asilimia 98.
Ameongeza kuwa ugonjwa huo pia umeathiri idadi kubwa ya watu waliokuwa wakifanya shughuli za utalii na kuzitegemea kwa ustawi wa uchumi wao kwa kukosa watalii ambapo amesema selta nyingine ambayo imeathirika na ugonjwa huo ni usafiri wa anga,uzalishaji,kilimo,biashara pamoja na sekta ya usafirishaji.
Marygoreth Mushi Afisa utalii Mwandamizi amesema kuwa sekta ya utalii ni moja kati ya sekta za kiuchumi zilizowahi kujibu masuala mbalimbali yanayohusiana na UVIKO 19 ambapo sekta binafsi ndiyo zipo kwenye uhalisia zaidi kwa kufanya biashara na ndiyo zinaotambua athari zaidi ambazo zinawapata moja kwa moja.
Ameongeza kuwa tangu mwaka 2020 wamekuwa wakijumuika na sekta binafsi ili kuona maeneo yaliyoahirika na namna ya kujikwamua ambapo wamekuwa wakifanya jitihada hizo kwa namna mbalimbali ikiwemo utambuzi wa maeneo ambayo sekta ya utalii yamekuwa yakiathirika kwa kiwango kikubwa,kutambua maeneo ambayo yanahitaji kufanyiwa muingiliano utakao pelekea kuwa na kiwango hatua za namna ya kujiendesha katika kipindi cha UVIKO 19.
“Tumekuwa tukishirikiana kwa ukatibu sana na wizara ya afya nchini kwa kuandaa utamaduni mpya wa kuweza kukabiliana na UVIKO 19 lakini pia uchumi hauwezi ukasimama,shughuli za kiuchumi zitakuwa bado zikiendelea na wakati zikiendelea shughuli hizo ni vitu gani hasa tunapaswa kuzingatia ili tuweze kuenenda na ambavyo dunia imekuwa ikibadilika.”alisema Bi.Marygoreth
Ameongeza kuwa katika hatua za karibuni wameweza kuja na mpango wa kuweza kurejesha sekta katika hali yake iliyokuwa awali kwani wanatambua na kuamini kwamba itachukuwa muda ambapo katika muda huo ni vitu gani ambavyo wanapaswa kufanya ili waweze kuendelea kuona manufaa ya utalii kama ilivyokuwa awali.
Naye mdau wa utalii ambaye ni katibu wa Taasisi ya waongoza utalii Tanzania TTGAwenye makao makuu jijini Arusha Bwn.Apolinary Kihwili amesema uwepo wao ni fursa kubwa ya kuwasaidia katika kupata mbinu sahihi za kuyumia mitandao ili kuweza kipata wageni na kutangaza biashara zao.
“Tunafanya utalii ili kupata kipato kitakachotusaidia kuendesha familia zetu hivyo tukitumia mitandao vizuri itatusaidia sana kuendesha na kuimarisha biashara zetu hasa baada ya janga la CORONA kutokea katika nchi yetu.”alisema Kihwili