Wanachama na wapenzi wa timu ya Simba SC mapema leo Asubuhi Septemba 18 ,2021 walijitokeza kufanya usafi Kwenye zahanati ya Tabata Kisiwani ikiwa ni sehemu ya shamrashamra kuelekea kwenye kilele cha Simba Day jumapili Septemba 19,2021.
Akiongoza shughuli hiyo mwenyekiti Tawi hilo ambaye pia ni mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Tabata Kisiwani Chala, amesema kuwa Tawi lao limeungana na matawi mengine kufanya shughuli za kijamii kwenye Zahanati hiyo nakwamba maandalizi yote ya wao kuwepo uwanjani hapo kesho yamekamilika.
“Maandalizi yote ya sisi kuwepo uwanjani kesho yamekamilika kwani tayari usafiri umepatikana wa kuwachukuwa wanachama na wapenzi kuwapeleka uwanjani na kuwarudisha sambamba na shamrashamra zote kufanyika hapa kuanzia Asubuhi” Alisema Chala.
Wanachama wa Tawi hilo la Wekundu wa Msimbazi la Tabata Kisiwani wameonekana kuhamasika kuweza kushiriki Tamaaha hilo la Simba Day litakalofanyika siku ya kesho likiambana na mchezo wa kirafiki kati ya Simba na TP Mazembe ya DRC kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Zifuatazo ni Picha Mbalimbali za Wanachama hao wakifanya usafi Zahanati ya Tabata Kisiwani.