NA: HERI SHAABAN (ILALA).
DIWANI wa Kata Kisukuru Lucy Lugome na wajumbe na Wajumbe wake wa Kamati ya Siasa Kata ya Kisukuru leo wamefanya ziara katika Kata hiyo kuangalia miradi ya Maendeleo ,ambapo Kamati ya Siasa walimpongeza Diwani Lucy kwa utekekezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Akizungumza katika ziara hiyo Diwani Lucy Lugome alisema anapata ushirikiano katika chama na Serikali katika usimamizi wa miradi yote ya Kata hiyo.
“Leo nimefanya ziara ya Kamati ya Siasa ya Kata yangu kuangalia utekelezaji wa Ilani na Maendeleo ambayo nimefanya ndani ya Kata hii kwa ushirikiano na chama na Serikali ” alisema Lucy .
DIWANI Lucy alisema tumekagua Kituo cha Polisi kuangalia Maendeleo yake pamoja na miundombinu ya Kata hiyo.
Diwani Lucy aliwataka Wajumbe wake wa Kamati ya Siasa kushirikiana kwa pamoja na Wananchi katika kuijenga Kata ya kisukuru iweze kuwa na Maendeleo .
Alisema changamoto za Kata hiyo atazitatua kwa kushirikiana Serikali pamoja na Mbunge wa Segerea Bonah Kamoli Diwani Lucy aliwataka wananchi wake wenye Changamoto mbalimbali kuwasiliana na Ofisi yake kwa ajili ya kuzitatua .
Mwisho