Home LOCAL BONAH AHAIDI FEDHA ZA JIMBO MILIONI 30 SEKTA ELIMU NA ULINZI

BONAH AHAIDI FEDHA ZA JIMBO MILIONI 30 SEKTA ELIMU NA ULINZI

Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli akizungumza na Diwani wa Kata ya Kiwalani Mussa Kafana leo September 22/2021 katika ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo wengine Viongozu wa Chama (PICHA NA HERI SHAABAN).

Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli akizungumza na Wanafunzi wa kidato cha kwanza Sekondari ya Kiwalani Wilayani Ilala leo September 22/2021 katika ziara ya Mbunge Bonah kukagua miradi ya Maendeleo (PICHA NA HERI SHAABAN).

Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli (kulia )akiwa na Diwani wa Kata ya Minazi Mirefu Godlisten Malisa leo September 22/2021 katika ziara ya Mbunge kukagua miradi ya Maendeleo ,ambapo Kata Minazi Mirefu Mbunge Bonah ameelekeza Shilingi Milioni Kumi fedha za Jimbo zijenge Kituo cha Polisi Jamii na Diwani Malisa amechangia shilingi 300,000/= kash kwa ajili ya ujenzi huo (PICHA NA HERI SHAABAN)

NA: HERI SHAABAN
MBUNGE wa Jimbo la Segerea Wilaya Ilala Bonah Ladslaus Kamoli, ameaidi  fedha za jimbo shilingi milioni 30 kwa ajili ya miradi ya Maendeleo ikiwemo Sekta ya Elimu na Ulinzi na Usalama.

Mbunge Bonah alitoa ahadi ya kugawa fedha za mfuko wa Jimbo leo katika ziara yake ya kukagua miradi ya Maendeleo na kutatua kero za wananchi Kata za Kiwalani, Minazi Mirefu ,Vingunguti na TABATA ambapo pia alipata fursa ya kuzungumza na Wananchi, Walimu na Wanafunzi.

“Leo nimefanya ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ndani ya Jimbo langu la Segerea katika baadhi ya Kata zenye changamoto nimezipatia fedha za Serikali ambazo zinazopitia mfuko wa Jimbo”
alisema Bonah

Katika ziara hiyo Mbunge alisema fedha za Jimbo la Segerea   shilingi milioni kumi zielekezwe  kwa ajili ya Kituo cha kisasa cha Polisi Jamii Mwale Kata ya Minazi Mirefu kwa ajili ya masuala ya ulinzi na Usalama  na kuagiza ifikapo January kiwe kimekamilika.

Pia Mbunge Bonah alisema fedha zingine  shilingi milioni 20 sekta ya Elimu shule ya Msingi Mwale Kata ya Kiwalani kwa ajili ya elimu, awali shule hiyo waliomba milioni 35 Ofisi ya Mbunge imeelekeza shilingi milioni 20.

Aidha Mbunge Bonah  aliwagiza Walimu Wakuu kujenga kwa kutumia (force  akaunti)na kuitumia fedha za Serikali kwa malengo sahihi kwa kushirikiana na Diwani wa Kata husika

“Fedha hii ya Serikali naomba hapa niwe mkali zitafika kwa wakati  itapitia akaunti za shule isitumike kinyume chake ” alisema.

Kwa upande wake Diwani wa Minazi Mirefu Godlisten Malisa alichangia shilingi laki 300,000/=kash kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi Mwale kwa ajili ya Masuala ya Ulinzi na Usalama.

Diwani Godlisten Malisa alisema anaunga mkono juhudi za Mbunge Bonah katika juhudi zake za kuleta Maendeleo atashirikiana na Mbunge katika kila jambo ndani ya Kata Minazi Mirefu na kuunga mkono Juhudi za Serikali.

Mbunge Bonah ziara yake pia akizungumza na wananchi wa Bonde la Msimbazi Tabata Mangaribi na  Vingunguti Wilaya ya Ilala.

Mwisho.

Previous articleMAGAZETI YA LEO ALHAMISI SEPTEMBA 23-2021
Next articleTASAC YATOA ELIMU KWA WANANCHI MAONESHO YA MADINI GEITA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here