Home LOCAL CHUPA ZA DAMU 288 ZAPATIKANA NDANI YA SIKU 10 MAONESHO YA MADINI...

CHUPA ZA DAMU 288 ZAPATIKANA NDANI YA SIKU 10 MAONESHO YA MADINI GEITA

Anaripoti, Pual Zahoro, Geita RS.

Mhe. Rosemary Senyamule Mkuu wa Mkoa wa Geita amesema mpaka leo Septemba 25, 2021 mpango wa kuchangia damu unaoendelea kwenye banda la damu Salama kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa na Waandishi wa Habari umefanikisha kupata chupa za damu 288 kutoka kwa wananchi mbalimbali waliojitolea kuchangia.

Mhe. Senyamule amesema hayo leo baada ya yeye mwenyewe kutoa damu kwenye Banda hilo huku akiungwa mkono na wananchi mbalimbali ambao kwa baada ya kusikia wito wake walihamasika na kuamua kusaidia kuokoa maisha ya wananchi kwa Jambo hilo. 



“Niwashukuru wote ambao wameshiriki kwa namna tofauti kuja kutoa damu zao niendelee kuwashukuru wote kuja kuendelea kutoa damu, nataka miseme wazi kwamba ndani ya siku ya 10 tangu maonesho ya Madini yalipoanza tumepata Chupa 288 mpaka sasa.” Mhe. Senyamule akipongeza.

“Natamani kuwa na wananchi wenye afya njema na nimeona sio jambo sahihi kuwahamasisha wengine alafu mwenyewe nisitoe damu na ndio maana nipo hapa leo na nimeshatoa damu, nawashukuru wote walioniunga mkono na ninamshukuru Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita kwa mchango wake Tshs. laki tatu alionipatia ili kufanikisha jambo hili.” Mkuu wa Mkoa.

“Mara nyingi Waandishi wa Habari tumekua tukiandika Habari za wananchi tena wengine wakiwa na matatizo mbalimbali ikiwemo kuishiwa damu sasa tukaona tusiishie kuripoti tu nasi tuwe sehemu ya msaada kwa kuchangia na kuhamasisha wengine kutoa damu.” Mutta Robert, Mwandisi wa Gazeti la Majira.





Previous articleRAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI
Next articleTANZANITE YAICHAPA ERITREA 3-0
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here