Home LOCAL RAIS SAMIA ANA MCHANGO MKUBWA YA MAENDELEO VISIWANI HUMO – MBELO

RAIS SAMIA ANA MCHANGO MKUBWA YA MAENDELEO VISIWANI HUMO – MBELO

Na: Halfan Abdulkadir, Zanzibar.

Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa Visiwani Zanzibar wamesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo ya visiwa hivyo.

Wakizungumza na Mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti, Wanasiasa hao wamesema Utawala wa Rais Samia ni wakupongezwa mno kutokana na jitihada zinazoendelea kuonyeshwa na kiongozi huyo ikiwemo kujenga Shule kupitia fedha za ahuweni za UVIKO 19, Hospitali za Wilaya, Masoko, vituo vya Ujasiriamali 14 vikivyotumia Bil 16 hadi kukamilika kwake.

Katibu wa Kamati maalumu NEC itikadi na uwenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar, Mbeto Khamis Mbeto amesema Rais Samia ametoa Shil Bil 18 Kwa ajili ya mikopo ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi.

“Tulitenga Bil 18 Ili Wananchi wapate kuwezeahwa kiuchumi,fedha hizo zilikuja kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mama (Rais Samia )akaagiza hizo fedha na Zanzibar ipate. Lakini ukiacha hilo tulitoa zaidi ya Boti 850 ambazo zilishatolewa Kwa ajili ya Wavuvi na wakulima wa Mwani” Alisema Mbeto.

Mbeto aliongeza kusema kuwa mchango wa Rais Samia Zanzibar hasa katika Serikali ya Awamu ya nane unaendelea kushuhudiwa ambapo Kuna mambo mengi ya maendeleo yanafanyika ikiwemo kuboresha ustawi wa jamii kwenye mambo mbalimbali nchini.

“Lakini ikikumbukwe Zanzibar ikapata fedha nyingine kwenye Mabadiliko ya tabianchi (Climate change) Asilimia 17 ya Fedha zile ambazo zilielekezwa zitumike huko” Alisema .

Pia Aliongeza ” Unajua 1964 tulipoungana, baadhi ya mamlaka ya Zanzibar yalikasimiwa na kusimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Zanzibar kama Zanzibar sio Dola haliwezi ikakopa, kwa Maana hiyo ikitaka mahitaji yake lazima ipitie kwenye Serikali ya Muungano. Lakini mara hii Mama ( Rais Samia) ameweka msisitizo kwa Kila jambo ambalo Zanzibar wanalitaka kuendesha uchumi wake na shughulii zake basi Serikali ya Jamhuri ya Muungano inachukua dhamana hiyo ikiwemo mikopo na mengineyo” Alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti Taifa wa Chama cha ADA TADEA Juma Ali Khatib amesema anampongeza Rais Samia Suluhu kwa Nia yake njema kuipaisha Zanzibar kiuchumi na kimaendeleo.

“Kiukweli Mama ni kiongozi hodari na mwenye maono mapana. Nampongeza sana. Amejenga vituo vya afya kwa wilaya zote za Unguja na Pemba. Mimi ni nimekuwa shahidi nimekagua hospital zote za wilaya, lakini pia zimejengwa shule za ghorofa kwa wilaya zote za Zanzibar “ Alisema Khatib.

Mwenyekiti huyo amesema katika miradi ya maendeleo, Zanzibar inashuhudiwa Ujenzi wa barabara kuelekea Mkoa Kusini unguja zikiwa katika Hali ya ubora na za kisasa.

Wanasiasa hao wametoa wito kwa Wananchi mbalimbali kumuunga mkono Kiongozi huyo wa nchi, na kuwapuuza wale waliowaita wapotoshaji na Wakosoaji wa Kila jambo la maendeleo linalofanywa nchini.

Previous articleWASIOJIWEZA WAISHUKURU SHUWASA KUWAPATIA HUDUMA YA MAJI BURE
Next articleWATUMISHI BRELA WAPATIWA ELIMU KUHUSU NHIF, WCF, UTT, WATUMISHI HOUSING, VYAMA VYA USHIRIKA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here