Na: Stella kessy, DAR ES SALAAM.
MSAFARA wa Baiskeli unatarajiwa kuanza jumapili kutoka Masaki mpaka Butiama kwaajili ya kuenzi miaka 22 tangu kifo cha Baba wa Taifa.
Akizungumza leo na waandishi wa habari Mkuu wa msafara wa huo Gabriel Landa amesema kuwa lengo la msafara huo ni kuenzi Baba wa Taifa kwa kuungana na watanzania wote.
Amesema kuwa msafara huo utaanzia katika makazi yake Msasani Dar es Salaam na kuhitimisha Mwitongo,Butiama kwa siku 14.
“Msafara huo ambao utatumia siku 14 kutoka Dar es Salaam mpaka Butiama zenye umbali wa kilometa zisipungua 1400 kupitia katika mikoa 10 wilaya 20 na kuhusisha washiriki wasiopungua 100”anasema.
Aliongeza kuwa watakuwa na washiriki zaidi ya 100 na wanategemea kuhitimisha msafara huko Mwitogo, Butuama wakiwa na washiriki zaidi ya 100 na ujumbe “changia dawati,tokomeza ujinga kwa maendeleo ya taifa”.
Aliongeza kuwa watanzania wataendelea kumuenzi Baba wa Taifa kwa mchango wake wa juu ya mapambano ya uhuru waafrika kutoka kwa serikali ya kikoloni ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha watanzania kuwa kitu kimoja bila kujali ukabila wala dini jambo linapelekea kudumisha mshikamano na amani kwa watanzania.
Alifafanua kuwa tangu kuanzishwa kwa msafara huu wa Twende Butiama 2018,msafara huu umekuwa unahamasisha watanzania kuendeleza juhudi za baba wataifa ikiwa ni pamoja na kupambana na maadui watatu wa maendeleo ambao ni Ujinga, Maradhi na umaskini.